Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( kulia) akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Busomeke( katikati) wilayani Igunga mkoani Tabora baada ya waziri huyo kuwasha umeme katika nyumba mwanakijiji huyo. |
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora
kuongeza kasi ya kutumia umeme unaopatikana mkoani humo kwakuwa matumizi
yao yapo chini zaidi kulinganisha na umeme unaozalishwa mkoani humo.
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati akikagua shughuli za usambazaji wa umeme vijijini katika Kijiji cha Mizanza na kuwasha umeme katika Kijiji cha Busomeke wilayani Igunga mkoani Tabora, Aprili 27, 2020.
Dkt. Kalemani alisema kuwa mitambo ya kufua umeme iliyopo mkoani humo inauwezo wakuzalisha Megawati 42 za umeme ili itumike mkoa mzima lakini mpaka sasa matumizi ni Megawati 14 tu.

“Kwa nini ninyi wakazi wa
Tabora hamtaki kutumia umeme haliyakuwa tayari miundombinu imewafikia
na bei ya kuunganisha ni 27,000 tu! mitambo ya hapa Tabora inauwezo wa
kufua umeme wa Megawati 42, ninyi matumizi yenu hayafiki hata nusu ya
umeme huo,hii si sawa mtaharibu mitambo yetu kwakuwa mingine italazimika
kuzimwa na ikizimwa kwa muda mrefu itaharibika na nchi itapata hasara”
alisema Dkt. Kalemani.
Aliwataka Viongozi wa Serikali za Vijiji, Mitaa pamoja na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuongeza kasi ya kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kuunganisha umeme katika nyumba zao.
Vilevile aliwataka wananchi hao kuongeza shughuli za uzalishaji mali kama vile viwanda vidogo vinavyotumia umeme ili kuongeza idadi ya matumizi ya umeme ambao mwingi hupotea kwa kukosa watumiaji hali yakuwa bado wakazi wengi hawana huduma hiyo.

No comments:
Post a Comment