Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo
ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kukamilisha mahitaji
muhimu ya Hospitali ya Wilaya hiyo ambayo iko katika hatua za ukamilishaji wa
ujenzi kwa tahadhari ya kupokea wagonjwa wa Korona endapo hali isipotengemaa.
Jafo
ameyasema hayo mapema leo alipotembelea Hospitali hiyo inayojengwa katika eneo
la Mlowo Wilayani Chamwino na kukuta ujenzi katika hatua za ukamilishaji kisha
kutoa rai hiyo kwa viongozi kujiandaa mapema na Janga hili la Kidunia.
Amesema
kutokana na Jiografia ya hospitali hii kuwa imejitenga kabisa na maeneo ya
makazi ya watu ninashauri muandae jengo moja maalumu na mlikamilishe kwa kila
kitu kinachohitajika ili endapo janga hili likiendelea jengo hilo litumika kwa
ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Korona.
“Kwa hali tuliyonayo sasa
hatutakiwa kukaa kusubiria mpaka hali iwe mbaya zaidi tunatakiwa kuendelea
kujikinga na kuchukua tahadhari za awali kabisa ikiwa ni pamoja na kuandaa
maeneo ya kutolea huduma kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu hatari na
hospitail yetu hii naona inafaa kabisa kwa kuwa ina sifa zote” alisisitiza
Jafo.
Wakati
huo huo Waziri Jafo aliwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Chamwino kwa
kusimamia kwa makini ujenzi wa Hospital hiyo na kuhakikisha kuwa inakamilika
kwa ubora wa hali ya juu na kwa wakati.
“Nimefurahi kukuta ujenzi umefikia
katika hatua hii ya ukamilishaji, vitu vidogo sana ndio vimebakia kumalizia
kabisa ujenzi na majengo yote yanaonekana kuwa na ubora wa hali ya juu hakika
nimefurahishwa na hatua hii na hongereni sana” Alisema Jafo.
Haya
kwangu mimi naona kama ni mafanikio kwani mwanzoni hali ilikua mbaya, ujenzi
ulikua unasuasua nilitumia nguvu kufuatilia na kusimamia lakini kwa sasa wote
tunajivunia mafanikio haya huu ndio uongozi wa pamoja unaotakiwa katika
utekelezaji wa miradi.
Hospitali
ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa HospitaIi za Halmashauri
71 zinazoendelea kujengwa Nchini Kote kupitia mpango wa Maboresho wa Huduma za
Afya unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Nteghenjwa Hosseah, Mlowo
No comments:
Post a Comment