|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Prof.
Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto . Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita ,
Aprili 22, 2020.
Rais Dkt. John Magufuli
amezungumza na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa Chato
Mkoani Geita kuhusu hali ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi
vya corona (Covid-19).
Mhe. Rais Magufuli
amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito wa kuchukua tahadhari dhidi ya
ugonjwa wa Corona, na kwa kushiriki katika siku 3 za kumuomba Mwenyezi Mungu
aepushe janga la ugonjwa huo.
|
|
Prof. Mabula
Daudi Mchembe akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato
Mkoani Geita , Aprili 22, 2020.
Rais Magufuli
amewapongeza Madaktari na Wauguzi walio mstari wa mbele katika kutoa huduma za
matibabu kwa wagonjwa wa Corona na ametoa wito kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhakikisha inachukua tahadhari za kutosha kwa
misaada ya vifaa vya uchunguzi wa Corona na vifaa vya kujikinga kuambukizwa au
kuambukiza (barakoa)
hasa baada ya baadhi yake kuhofiwa kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo.
Pia ametoa wito kwa
wenye viwanda hapa nchini kuzalisha barakoa kwa ajili ya Watanzania na vifaa
vingine vya kukabiliana na ugonjwa huo yakiwemo mavazi ya watoa huduma na
mashine za kupumulia kwa wagonjwa badala ya kutegemea vifaa hivyo kutoka nje ya
nchi pekee.
|
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi
vitendea kazi Prof. Mabula Daudi Mchembe mara baada ya kumuapisha kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla
iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020.
|
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020.
Rais Magufuli
amewataka viongozi kujihadhari na baadhi ya njia zinazotumika kukabiliana na
ugonjwa huo, ikiwemo kupulizia mitaa na majengo kwa kutumia kemikali zisizokuwa
na uwezo wa kuua virusi vya Corona kama ilivyofanyika kwa baadhi ya Mikoa hapa
nchini, na badala yake amewataka viongozi hao kusisitiza njia za uhakika za
kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha, Mhe. Rais
Magufuli amesema Serikali haitawafungia wananchi majumbani (lockdown)
wala kulifunga Jiji la Dar es Salaam ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza
kuwakumba wananchi na kuathiri uchumi wa nchi, na ametaka Watanzania kuondoa
hofu, kuendelea kuchukua tahadhari huku wakiendelea na shughuli zao za
uzalishaji mali na ujenzi wa Taifa.
|
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. |

“Tuwaondoe hofu wananchi, sio
ugonjwa huu pekee unaosababisha vifo kwa wananchi, na sio kila anayepoteza
maisha hivi sasa basi amekufa kwa Corona, nimejulishwa takwimu za mpaka jana
idadi ya walioambukizwa ni 284 na kati yao takribani 100 wamepona, tuwaambie
wananchi kuhusu taarifa hizi badala ya kuwaacha wanajawa na hofu hali inayoleta
madhara zaidi” amesema Rais Magufuli.
Amewataka Viongozi
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
wanaosababisha hofu kwa wananchi na kusambaza taarifa zisizo sahihi wakiwemo
Wanasiasa ambao amewaonya kuacha kutafuta umaarufu wa kisiasa kupitia janga
hili, na badala yake Watanzania wote waungane kupambana nalo.
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. |
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. |
Rais Magufuli
ametoa wito kwa nchi zote za Afrika kuungana kuziomba taasisi za kifedha za
kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia ambazo zimetangaza kusaidia Mataifa ya Afrika,
kutoa msamaha wa madeni badala ya kutaka kukopesha mikopo mingine ilihali nchi
hizo zinakabiliwa na madeni ya mikopo ya zamani.
Amewatakia Waislamu
wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao unatarajiwa kuanza siku
chache zijazo na ametoa wito kwao kutumia mfungo huo kumuomba Mwenyezi Mungu
aepushe janga la ugonjwa wa Corona.
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. |
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. |
|
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona
nchini, ambapo kabla ya kikao hicho Mhe. Rais amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .Hafla iliyofanyika
Wilayani Chato Mkoani Geita , Aprili 22, 2020. PICHA NA IKULU
Mapema kabla ya
kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Prof. Mabula Daudi Mchembe kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Prof. Mchembe
amechukua nafasi ya Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula ambaye amehamishwa na kuwa
Katibu Mkuu wa Mawasiliano.
Mhe. Rais Magufuli amesema
amefanya mabadiliko hayo ili kuongeza kasi ya utendaji katika Wizara ya Afya
ikiwemo kukabiliana na ugonjwa wa Corona
|
No comments:
Post a Comment