Baadhi ya wajumbe
wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili
katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo
tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu,
Dodoma, kulia ni, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Jim Yonazi na (kushoto) ni Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo , Dkt. Hassan Abbas
(katikati).
|
Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea na zoezi la kuratibu awamu ya pili
ya uendelezaji wa mji wa serikali eneo la Mtumba, makao makuu ya nchi jijini
Dodoma. Awamu hii ya pili inahusisha Ubunifu na ujenzi wa majengo makubwa ya
Ofisi zitakazotumiwa na Wizara za serikali.
Akiongea, leo tarehe 20 Aprili, 2020, katika kikao cha Kamati ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu , Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda, amefafanua kuwa awamu hii ya pili ya mpango huo inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.
Akiongea, leo tarehe 20 Aprili, 2020, katika kikao cha Kamati ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu , Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Tixon Nzunda, amefafanua kuwa awamu hii ya pili ya mpango huo inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe
wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili
katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma,
wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa
Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma.
|
Aidha, kufanikiwa
kwa mpango huo ni kutachangiza jiji la Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa
linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma
hiyo, tayari Timu ya Wataalam imepitia michoro ya ubunifu na usanifu. Pia
Wakala wa majengo Tanzania (TBA), inaendelea kufanya kazi kwa karibu na Taasisi
nyingine zinazohusika na miundo mbinu katika mji wa Serikali kama vile TARURA,
DOWASA, TANESCO, ZIMAMOTO, TPDC, TTCL na eGA.
Baadhi
ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi
wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20,
Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri
Mkuu, Dodoma.
Mwenyekiti
wa Timu ya Kutengeneza Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma Prof. John Lupala
akiwasilisha mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili
katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakati wa kikao kazi cha makatibu
Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao
kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili,
20,2020, lengo ikiwa ni kujadili mpango
kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa
Serikali Mtumba Dodoma, Kikao kimefanyika katika Ukimbi wa Mkutano wa ofisi
yake Dodoma.
Hivi karibuni ,
Mwezi Februari mwaka huu, 2020, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
alizindua Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo aliwataka
wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa kiwango cha juu katika utekelezaji wa
Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kulifanya kuwa
jiji bora na la kisasa nchini.
Serikali, kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za
Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016.
Uamuzi wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni
maelekezo ya Chama cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
No comments:
Post a Comment