Matokeo chanyA+ online




Sunday, April 19, 2020

MFUMO WA UKATISHAJI TIKETI KWA NJIA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI

Serikali imesema kuwa mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao utaanza kutumika hivi karibuni kwa mabasi yote yanayofanya safari zake mikoani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandishi Isack Kamwelwe

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandishi Isack Kamwelwe, wakati wa akikaguzi wa mifumo hiyo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo itafikiwa hivi karibuni kwani kiu ya serikali ni kuona wananchi wananufaika kwa na huduma hiyo.
Mbali na mabasi  hayo ya mikoani, daladala pamoja na mabasi ya mwendokasi yanatarajiwa kuuganishwa katika  mfumo huo ambao utarahisisha huduma na kuondoa adha ya wapiga debe vituoni. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Waziri Kamwelwe amesema serikali imefikia hatua ya mwisho ya kuanza kutumika kwa mfumo huo ambapo wananchi watatumia simu kukata tiketi za mabasi na hawatolazimika kutembelea vituoni jambo litakalowaepusha na wizi unaofanywa kupitia ulanguzi wa tiketi na wapiga debe.

“Nimeridhishwa na mfumo, huu ambao utasimamiwa na serikali kupitia kituo chetu cha National Internet Data center(NIDC) ukweli utasaidia sana wananchi wetu hususani wale wa chini ambao walikuwa wanaingia gharama kwenda katika vituoni kukata tiketi, tumefika wakati wa kuwa kisasa zaidi wapiga debe walikuwa wakiongeza gharama lakini wakati huu wa maambukizi ya corona ni muhimu kutafuta njia mbadala katika usafirishaji,”alisema.

Mhandisi Kamwelwe amesema, ameridhaka na uandaaji wa kimifumo kwakuwa taarifa zitatunzwa vizuri na kufanya kazi kwa ushirikishi wa wadau wa usafiri nchini.

“Hakuna sababu ya msafiri kutembea na pesa mkononi, hata wanaopandia njiani ni wakati wa kuwa na pesa kwenye simu, kwakuwa hatuna uhakika iwapo ugonjwa huu utaenea hadi kwenye noti ni lazima kuwa na njia nyingi za udhibiti,”alisema

Amesema wamiliki wa mabasi walikuwa na maswali mengi wakati wa mchakato wa mfumo huo, wakihofia kupata hasara lakini ni wazi utendaji wake utanufaisha pande zote.

No comments:

Post a Comment