 |
|
Muonekano wa Jengo la
utawala katika Hospitali ya Wilaya ya Uyui
Mkoani Tabora baada ya ujenzi wa
Hospitali hiyo kukamilka tayari kwa kuanza kutoa huduma, ujenzi wa Hospitali
hiyo umegharimu shilingi Bilioni 1.5 hadi kukamilika.
|
Serikali ya Awamu ya
Tano imetimiza ndoto ya wananchi wa Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora kufikiwa na
huduma bora za afya katika maeneo yao.
Akizungumza katika mahojiano
maalum wilayani humo, Mkuu wa Wilaya, Gift Msuya amesema kuwa kwa sasa wananchi
wa wilaya hiyo wanafikiwa na huduma za afya kupitia vituo vya afya
vilivyojengwa na vile vilivyoboreshwa katika kipindi cha miaka mine iliyopita.
 |
|
Sehemu ya majengo ya
Hospitali ya Wilaya ya Uyui Mkoani
Tabora baada ya ujenzi wa Hospitali hiyo kukamilka tayari kwa kuanza kutoa
huduma, ujenzi wa Hospitali hiyo umegharimu shilingi Bilioni 1.5 hadi
kukamilika.
“Tumekamilisha ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya iliyogharimu Shilingi bilioni 1.5 na iko tayari kuanza
kutoa huduma baada ya kuwasili kwa vifaa, hili linaenda sambamba na utoaji wa
huduma katika vituo vyetu vya afya ambavyo vinatoa huduma zinazoendana na
mahitaji ya wananchi,” alisisitiza Msuya
Aidha, Msuya amesema
kuwa Serikali ilitoa milioni 500 zilizowezesha kuboreshwa kwa Kituo cha Afya
Upuge na pia shilingi milioni 400 zimetumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya
Igalula.
|
 |
|
Muonekano wa Chumba cha
Upasuaji katika kituo cha Afya Upuge Wilayani Uyui baada ya kuboreshwa kwa
gharama ya shilingi milioni 500 zilizotumika kujenga majengo mapya
yaliyowezesha huduma kuboreshwa ikiwemo kuanza kwa huduma za upasuaji.
Kuwepo kwa huduma bora
na vifaa vya kisasa kumewezesha Wilaya ya Uyui kutokuwa na vifo vya akinamama
wanaopatwa na uchungu pingamizi kwa kuwa sasa huduma ya upasuaji inapatikana
karibu na walipo wananchi tofauti na ilivyokuwa awali.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi
wa Kituo cha Afya Upuge, Sr. Dkt. Yustina Raphael amesema kuwa tangu kuanza kwa huduma ya upasuaji
kwa akinamama zaidi ya akinamama 100 wamefanyiwa upasuaji kwa ufanisi.
“Jukumu letu ni
kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia kituo hiki cha Upuge kwa kuwa
kimeboreshwa na kina vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ikiwemo vya maabara na
vya kufanyia upasuaji,” alisisitiza Sr. Dkt. Yustina
Awali, kabla ya
maboresho ya kituo hiki kilichoanza
mwaka 1977 kilikuwa na huduma chache na kwa sasa kimeongeza huduma kama za
maabara, upasuaji, mama na mtoto na pia watumishi wameongezwa ili kuendana na
mahitaji.
|
 |
|
Sehemu ya majengo mapya
ya Kituo cha Afya Upuge Wilayani Uyui Mkoani Tabora kama yanavyoonekana baada
kuboreshwa kwa gharama ya shilingi milioni 500 zilizotumika kujenga
majengo mapya yaliyowezesha huduma kuboreshwa ikiwemo kuanza kwa huduma za
upasuaji.(Picha zote na Aboubakari
Kafumba)
Na
Frank Mvungi- MAELEZO
Akizungumzia kuhusu
rufaa katika Kituo hicho, Sr. Dkt. Yustina amesema kuwa baada ya maboresho
rufaa za wagonjwa zimepungua kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwapunguzia wananchi
adha ya kutembea umbali mrefu au kusafiri kufuata huduma za afya.
Kwa upande wake mmoja
wa wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo hicho, Bi. Salma Ramadhani
aliwapongeza watoa huduma wa kituo cha afya Upuge kwa utendaji bora na wenye
tija kwa wananchi wote wanaofika kupata huduma
kituoni hapo.
“Tunamshukuru Mhe. Rais
Magufuli kwa kuboresha sekta ya afya hasa vituo vyetu vya afya kama hiki cha Upuge kwa sasa tunapata huduma
za upasuaji hapa na wahudumu wa hapa wakiwemo madaktari wanatuhudumia vizuri na
mazingira yameboreshwa kupitia majengo mapya na vifaa vya kisasa kabisa”, alisisitiza
Salma.
Akifafanua amesema
kuwa amefanikiwa kujifungua salama
kutokana na huduma bora zilizopo katika kituo hicho hali inayowafanya akinamama
kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Serikali ya Awamu ya
Tano imefanikiwa katika kuimarisha huduma za afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya
afya, hospitali za wilaya, zahanati, ujenzi wa hosptali za rufaa za Mikoa na
Kanda na pia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba imekuwa chachu ya kuboreshwa kwa
huduma katika wilaya na mikoa yote hapa nchini.
|
No comments:
Post a Comment