Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. |
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara mkoani Morogoro na kumwagiza
Mkandarasi, Kampuni ya State Grid, anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, mkoani
humo kumaliza kazi kwa wakati.
Mgalu
alilazimika kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko ya kusuasua kwa
Mradi husika ambapo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi huyo ili kuhakikisha
anakamilisha kazi kwa muda ulioainishwa kwenye Mkataba.
Wakati
wa ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25 mwaka huu, Naibu Waziri alitembelea baadhi
ya vijiji vya Wilaya za Gairo na Mvomero kujionea maendeleo ya kazi husika.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati-mwenye ushungi), akikagua kazi ya kuunganisha umeme vijijini inayoendelea katika eneo la Ukwamani, wilayani Gairo hivi karibuni. |
Vijiji
vilivyotembelewa ni Ukwamani na Nguyami (Gairo) pamoja na Komtanga (Mvomero).
Kadhalika, Naibu Waziri alitembelea Yadi ya Mkandarasi iliyopo Gairo Mjini.
Naibu
Waziri aliwaasa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuchukua
tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na virusi vya Corona huku
wakiendelea kufanya shughuli zao.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikagua Yadi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, wilayani Gairo, akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. |
Pia,
aliwataka TANESCO Mkoa wa Morogoro kuhakikisha wananchi wote wanaolipia ili
kuunganishiwa umeme, wanapatiwa huduma hiyo kwa wakati.
No comments:
Post a Comment