Mkuu wa Idara ya Usingizi na Ganzi wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Phillip Muhochi (kulia) akimkabidhi cheti
mhitimu wa mafunzo ya mwaka mmoja ngazi ya cheti ya kozi ya usingizi na
ganzi Bw. Israel Mwasenga.
Wataalamu sita wa tiba ya usingizi na ganzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamehitimu mafunzo maalum ya mwaka mmoja ya ngazi ya cheti yaliyolenga kuwapatia ujuzi kuwapatia ujuzi wa namna ya kuhudumia wagonjwa wanaohitaji tiba hiyo.
Mafunzo hayo ambayo yametolewa na Hospitali ya Muhimbili kwa njia ya nadharia na vitendo kwa wataalamu ili kuwaongezea ujuzi na kisha kufanya mitihani mbalimbali ili kupima uwezo wao iwapo wanakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kutoa huduma.
Mkuu wa Idara ya Tiba ya Usingizi na Ganzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Phillip Muhochi amesema kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa kuzingatia viwango stahiki na kuwapatia wataalamu nafasi ya kwenda MNH-Upanga kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi.
“Mafunzo haya ya nadharia na vitendo yametolewa kwa viwango vya juu na kuwaruhusu wataalamu hawa kuzungukia maeneo ya mafunzo kama vile MNH-Upanga ili kuwapa uwanja mpana wa wao kujifunza na kupata ujuzi zaidi” amesema Dkt. Muhochi.
|
No comments:
Post a Comment