Matokeo chanyA+ online




Saturday, April 25, 2020

RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,973

Rais Dkt. John Magufuli amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dkt. John Magufuli

Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku ya kesho (26 Aprili, 2020) kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona.

Katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano, Mhe. Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yake wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao, na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Mhe. Rais Magufuli amesema ana matumaini kuwa wafungwa hao wamejifunza na watajirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria na taratibu.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19) ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment