Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza |
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati
yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000
za Wajane mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko
yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi
waliojenga mabondeni kuondoka.
RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.
RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza |
Aidha
RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo
ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa
kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya
nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana
na Mafuriko ya Mara kwa Mara.
Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Nyumba mbalimbali zilizoathiriwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar na Kwingineko nchini |
Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.
RC Makonda pia amewaelekeza wakandarasi kutumia kipindi hiki cha mvua kuangalia kama Design ya madaraja wanayojenga yanakidhi kuhimili na kupitisha maji ya mvua ili wabuni design mpya zinazokidhi viwango.
No comments:
Post a Comment