 |
Muonekano wa moja ya Vichwa
vya treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) vilivyokamilika
baada ya kufungwa mashine ya kufua umeme (Tranction Motor), katika karakana ya
Mamlaka hiyo Mkoni Mbeya
|
 |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Karakana ya Mamlaka ya Reli ya
Tanzania na Zambia (TAZARA) Mbeya, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, mara baada ya
kukagua vichwa viwili vya treni ya shirika hilo vilivyofungwa mashine ya kufua
umeme (traction motor) mpya.
|
 |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Isack Kamwelwe, akinawa mikono kama njia ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi
vya Korona katika Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
mkoani Mbeya.
Serikali ya Tanzania imetoa kiasi cha shilingi bilioni
10 ikiwa ni kuhakikisha inaifufua upya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) ili kuiongeza mtaji na kufikia lengo la kujiendesha kibiashara.
Akizungumza mkoani Mbeya mara baada ya kukagua vichwa
viwili vilivyokamilika baada ya kufungwa mashine mpya za kufua umeme (traction
motor) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema
kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutaongeza usafirishaji wa mzigo kwa mamlaka.
|
 |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Isack Kamwelwe, akimsikiliza Meneja wa Karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania
na Zambia (TAZARA) Mbeya, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, wakati akimweleza hatua
ya ukarabati iliyofikiwa katika karakana ya tazara mkoani Mbeya.
|
“Makusudi makubwa ya Serikali kuwekeza fedha hizi ni
kuhakikisha mnafanya biashara na kurejesha mzigo wa tani milioni tano
mnaotakiwa kuusafirisha kwa mwaka”, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Kamwelwe amefafanua kuwa fedha hizo zilizotolewa
zimeshanunua mashine mpya za kufua umeme takribani arubaini na mbili ambazo
zitafungwa kwenye vichwa saba.
 |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Isack Kamwelwe, akizungumza na wafanyakazi wa karakana ya maelekezo Karakana ya
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya (hawapo pichani)
wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa vichwa vya treni mkoani humo.
Meneja Karakana ya TAZARA mkoani humo, Mhandisi
Ezekiel Mong’ateko, amesema mpaka sasa vichwa viwili vimeshakamilika na mwishoni
mwa mwezi huu kichwa cha tatu kitakamilika ambapo kichwa kimoja kina uwezo wa
kusafirisha tani laki mbili na nusu kwa mwaka.
“Kukamilika kwa vichwa hivi kutaongeza mzigo tunaotakiwa
kuusafirisha kwa mwaka kwani kwa sasa mzigo tunasafirisha umepungua sana na hauzidi
tani laki tatu, tunaishukuru sana Serikali kwa kuiwezesha mamlaka”, amesema
Mhandisi Mong’ateko.
|
 |
Muonekano wa vifaa vinavyofanyiwa ukarabati katika
karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mkoani Mbeya.
|
Mhandisi Mong’ateko ameongeza kuwa sambamba na
ukarabati wa vichwa hivyo mkoani humo, Mamlaka inaendelea na ukarabati wa mabehewa
katika karakana ya mamlaka jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha ukamilikaji wa
vichwa hivyo unaendana na ongezeko la usafirishaji wa abiria na mizigo.
 |
Mafundi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) mkoani Mbeya, wakiendelea na ukarabati wa vichwa vya treni katika
karakana hiyo mkoani humo. TAZARA iko katika hatua za mwisho za kukamilisha
ukarabati wa kichwa cha tat umara baada ya kufunga traction motor mpya.
|
Kukamilika kwa ukarabati wa vichwa hivyo kutaongeza
idadi ya vichwa kumi na tatu vilivyopo kwa sasa na kufikia vichwa 20 ambapo
kila kichwa kina uwezo wa kubeba tani elfu thelathini.
Utoaji wa fedha hizo ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi
Mbili ya Tanzania na Zambia ambazo kwa pamoja zilikubaliana kutoa bilioni 20 ambapo
kila nchi ilitakiwa kuchangia bilioni kumi ili kuifufua upya mamlaka hiyo na
kuiwezesha kujitegemea mara baada ya kushuka kwa usafirishaji kutokana na
upungufu wa vichwa.
No comments:
Post a Comment