 |
Baadhi ya Wataalam wakiwa juu ya “Kinu”
walikopatiwa maelezo na Mzee Kisangani (wa mwisho) kuona namna kinavyofanya
kazi. Wa kwanza ni DKt. Yohana Mtoni (NDC), Prof. Sylivester Mpanduji (SIDO),
Prof. Madundo Mtambo (TIRDO) na Leo Mavuka (TAMISEMI).
Timu iliyoundwa na
Waziri wa Madini Doto Biteko imekamilisha maagizo iliyopewa baada ya kuwasili
Mkoani Njombe kwa Mzee Kisangani. Maagizo hayo ni pamoja na kuangalia changamoto
za jumla zinazomkabili Mjasiriamali huyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya
Kijasiriamali.
Changamoto hizo ni
pamoja na ukosefu wa upatikanaji wa Nishati ya Makaa ya Mawe ya kuyeyushia
madini ya chuma, Mtaji wa kuendeshea kiwanda, ukosefu wa leseni za kuchimbia
madini ya chuma, eneo la kiwanda cha kutengenezea zana za Kilimo na eneo la
kuyeyushia Madini ya chuma, miundombinu mbalimbali.
|
 |
Mzee Kisangani akiwa Kiwandani kwake
anakotengenezea zana mbalimbali zinazotumika Mashambani.
|
 |
Sehemu ya Kiwanda (Kinu) cha Mzee
Kisangani cha Kuyeyushia Madini ya Chuma kabla ya kupelekwa Kiwandani kwa ajili
ya kutengeneza zana za Kilimo.
Akizungumza jana, Aprili
13, 2020 mkoani Njombe, mara baada ya kukamilisha kazi hiyo, Mwenyekiti wa timu
hiyo, Prof. Sylivester Mpanduji alisema, timu yake imekamilisha shuguli zote
kwa mujibu wa hadidu za rejea walizopewa.
Ameongeza kuwa, timu
yake imefurahishwa na shuguli za Mzee Kisangani. Alisema, licha ya kwamba Kisangani
hajasoma hata darasa moja na hana Teknolojia ya kisasa lakini amebuni na
kutengeneza umeme wa kuendeshea kiwanda chake, kutengeneza kinu cha kuyeyushia
madini ya chuma na kuunda kiwanda cha kutengenezea zana zinazotumika mashambani
kama vile, Fyekeo, Mapanga, Reki, Visu,Shoka.
|
 |
Timu ya Wataalamu wakipitia kwa pamoja taarifa
ya ripoti kwenye ofisi za Tume ya Madini
mkoani Njombe, kabla ya kuiwasilisha kwa
Waziri wa Madini Doto Biteko.
|
Mmoja wa wataalam,
kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshugulikia
masuala ya Uchumi na Miradi, Leo Mavuka alisema, ipo sababu ya Serikali kuwaongezea
nguvu watu wenye ubunifu ili kuinua uwezo wao na kupanua maarifa waliyonayo ili
ubunifu wao usaidie jamii inayo wazunguka kama anavyofanya Mzee Kisangani.
Akizungumzia historia
yake, Mzee Kisangani alisema kazi ya Uhunzi alianza mwaka 1991 akiishi na marehemu
kaka yake Vicent Mtitu ambae pia alikuwa Muhunzi. Mwaka 1996 alianza shuguli
zake rasmi kwa kujitegemea kazi za Uhunzi. Tangu awali waliendelea kufanya kazi
zao bila teknolojia ya kisasa. Walitengeneza zana mbalimbali kwa kutumia
teknolojia ndogo kwa kutumia ubunifu.
Amesema, tangu afike Waziri
wa Madini Doto Biteko Machi 13-16 mwaka huu mkoani Njombe, baadhi ya changamoto
zimeanza kutatuliwa hususani upatikanaji wa Nishati ya Makaa ya Mawe, ujio wa
Kamati ya kuangalia shuguli zake na upatikanaji wa leseni za uchimbaji wa
madini ya chuma.
No comments:
Post a Comment