Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shughuli za maendeleo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Serikali
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli
imeendelea kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula ili watu
wake wawe na nguvu ya kufanya kazi kufikia uchumi wa viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Kauli hii ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Tarehe 11 Aprili 2020 mkoani Songwe wakati akikagua mashamba ya wakulima mashambani.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya PCT Ndg John Power wakati akikagua eneo maalumu lililopemndekezwa na kampuni hiyo kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu za Pareto wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Akiwa
katika Kijiji cha Idiwili na Iyula mkoani humo Waziri Hasunga
ameridhishwa na hali ya ustawi wa mazao ya wakulima shambani hivyo
kuwahakikishia wananchi kuwa kutakuwa na mavuno ya kutosha katika msimu
wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kwani wakulima wengi wameitikia wito wa
serikali wa kuongeza tija na uzalishaji wa mazao.
Waziri
Hasunga amesema kwa miaka mitatu sasa serikali ya imeendelea
kuhakikisha nchi inazalisha mazao mengi na ya kutosha ya chakula
kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wizara ya kilimo na taasisi zake.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo wakati akikagua shughuli za maendeleo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Alibainisha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula mwaka 2019 ulishuka ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo nchi ilizalisha tani milioni 16.8 hivyo katika msimu huu wa mwaka 2020 nchi itazalisha mazao ya kutosha na kuwa na utoshelevu mkubwa wa chakula
Amewapongeza
wakulima nchini kwa kuitikia wito na maelekezo ya serikali katika
kuhakikisha uzalishaji nchini unaendelea kuongezeka hususani kwenye mazao ya chakula na biashara.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua maendeleo ya mazao shambani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga ameigiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
Tanzania (TFRA) kuhakikisha inaharakisha upatikanaji na usambazaji wa
mbolea aina ya UREA ambayo imeadimika kwa wakulima.
Katika
hatua nyingine Waziri Hasunga amebainisha mkakati wa serikali wa
kuongeza uzalishaji wa zao la Pareto ambapo umeanza mkakati wa makusudi
wa kuanzisha shamba la pareto katika Kijiji cha Idiwili Mkoani Songwe kwa ajili ya uvunaji wa mbegu ili kuongeza kiasi cha mbegu kwani idadi ya wakulima inaongezeka kila siku.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shughuli za maendeleo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe tarehe 11 Aprili 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Tanzania imejaaliwa kuwa na mifumo mbalimbali ya kilimo yenye misimu ya tabia nchi inayotofautiana na hali za ekolojia ya kilimo inayofaa kwa uzalishaji wa mazao. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mahindi, mtama, lulu, mpunga, ngano, jamii ya kunde (hasa maharage), mihogo, mbatata, ndizi mbichi na ndizi za kuiva. Vyakula mbalimbali vya biashara vinavyozalishwa ni pamoja na kahawa, pamba, korosho tumbaku, katani, pareto, chai na miwa.
Mbegu za mafuta ni pamoja na karanga, alizeti na ufuta. Kilimo cha bustani hujumuisha mazao kama vile mbogamboga, matunda, maua na viungo vya chakula. Karafuu ni zao kuu la biashara kwenye visiwa vya Zanzibar
No comments:
Post a Comment