Chuo
Kikuu cha Dodoma(UDOM ) kupitia wataalamu wake, kimeanza kutengeneza
Barakoa na Vitakasa mikono kwa lengo la kuongeza nguvu na mchango wa
Chuo hiko katika kusaidia kupambana na maambukizi ya Virusi vya Homa
kali ya mapafu (COVID 19) hapa nchini.
Majengo ya Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)iliyoteuliwa kupokea wa Corona |
Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Faustine Bee amemwambia Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Binilith Mahenge aliyeambatana na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Dodoma kuwa, Chuo hicho kitaanza kusambaza vifaa
hivyo kwa wingi na kwa gharama nafuu ambayo watu na Taasisi wataimudu.
"Kama chuo tumeona tusaidie katika mapambano haya,tutazalisha barakoa na vitakasa mikono kwa bei nafuu,"alisema Mkuu huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge akiwasili hospitali ya UDOM akiwa katika ziara na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wataalam wa afya mkoa. |
Katika
hatua nyingine Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana
na Uongozi wa UDOM umeiteua hospitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma kuanza
kutumika kutoa huduma za matibabu kwa Wagonjwa wa Corona.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt Mahenge kwa kushirikiana na Timu ya wataalamu wa Afya wa Mkoa
wa Dodoma na uongozi wa UDOM umefanya ziara ya kukagua hospitali ya
Chuo hicho na kujiridhisha kuwa itasaidia kuboresha na kuimarisha utoaji
huduma kwa wagonjwa watakaothibitika kuugua Corona.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge akipokea maelezo ya moja wa wodi iliyopo Hospitali ya UDOM kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Alex Ernest. |
Hospitali
hiyo inafanya idadi ya hospitali za kutolea matibabu ya Corona kwenye
Wilaya ya Dodoma kuwa mbili ikiwemo Kituo cha Afya Mkonze.
No comments:
Post a Comment