Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi magari 10 ya kubebea wagonjwa kwa
wabunge ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za dhati za Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha
Watanzania wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao.
Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya sh. bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund. Kati ya magari hayo, 18 yatapelekwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa na 32 ni kwa ajili ya hospitali za Halmashauri pamoja na vituo vya afya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde
wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye
thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo
yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wa tatu kulia ni Mbunge wa Nyasa ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi, Stella Manyanya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) wakifurahia wakati Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (kulia) alikionyesha ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhiwa wakati Waziri Mkuu alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kulia) wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ulanga, Goodluck
Mlinga wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge
yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano
hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma. Katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea shukurani kutoka kwa Mbunge wa
Mbulu Vijijini Fratei Massay wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea
wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29,
2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri
Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Aprili 29, 2020) kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Ambapo amesema mbali na magari hayo kutolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za mama na mtoto pia yatatumika kuwahudumia wagonjwa wa corona ili kuokoa maisha ya wananchi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) wakifurahia wakati Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta (kulia) alikionyesha ufunguo wa gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhiwa wakati Waziri Mkuu alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (kulia) wakati alipokabidhi magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge yenye thamani ya shilingi bilioni 6, Aprili 29, 2020. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Aprili 29, 2020) kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Ambapo amesema mbali na magari hayo kutolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za mama na mtoto pia yatatumika kuwahudumia wagonjwa wa corona ili kuokoa maisha ya wananchi.
“Eneo hili tumeliwekea nguvu za kutosha na Watanzania wote ni mashahidi kwa namna ambavyo Serikali imejitahidi sana katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kwenye jamii zetu. Magari haya yatakwenda kutumika kwa ajili ya mama na mtoto lakini kwa kuwa gari litakuwepo kituoni litawahudumia na wagonjwa wengine.”

“Magari haya yatakwenda kufanya kazi ya kuokoa maisha ya Watanzania wengi kwa kuwasafirisha wagonjwa wa rufaa kutoka kituo cha afya kwenda hospitali ya wilaya na hospitali ya wilaya kwenda hospitali ya rufaa.”
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ununuzi wa magari hayo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuboresha zaidi huduma afya kwa wananchi.

“Watanzania wameshuhuduia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli, wameshuhudia upatikanaji wa dawa, wameshuhudia maboresho makubwa katika upatikanaji wa vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hosptali za halmashauri pamoja na hospitali za rufaa za mikoa na uboreshwaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya.”
Akizungumza kwa niaba ya wabunge waliopokea magari hayo, Mbunge wa Ileje, Janneth Mbenne amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kitendo hicho cha kihistoria.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa mawazo na maono makubwa ya maendeleo
ya Taifa. Magari haya yatakwenda kuboresha huduma za afya katika majimbo
yetu.”
Naye Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2015-2020 kwa vitendo. “…moyo usio na shukurani hukausha mema yote na heri wale wanaowajali wagonjwa kwa maana ufalme wa Mungu ni wao.”
Pia, Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Nyasa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msaada huo kwani walikuwa na changamoto kubwa na gari la kubebea wagonjwa.

No comments:
Post a Comment