 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu akitoa maelekezo alipotembelea eneo la bahari
kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya
wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam
wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji
kujaa.
|
 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu (mwenye kofia) akiwa ameambatana na wataalamu
wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
akiwa katika ufukwe alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro uliotokana na
changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White
Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa
udongo na hivyo maji kujaa.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu amewataka wataalamu wa mazingira kufanya
tathmini ya mazingira katika maeneo ya bahari kupata dawa ya madhara
yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Zungu alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika eneo la
bahari lenye mgogoro kati ya Motison wanaomiliki hoteli ya Whitesand
wakituhumiwa na wamiliki wa hoteli ya Wellworth Kunduchi kwa kujenga ukuta
baharini hatua iliyosababisha maji kujaa hotelini kwao.
 |
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka akimpa
maelekezo Afisa Sheria na Utawala kutoka hoteli ya Wellworth, Saimon Nguka
kuhusu kufanya Tathmni ya Athari za Mazingira (EIA) wakati wa ziara ya Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Azzan Zungu
katika eneo hilo jijini Dar es Salaam alipofika kusikiliza na kutatua mgogoro
uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth
na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha
mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.
|
Akizungumza katika eneo hilo akiwa ameambatana na watendaji
kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) waziri huyo aliwataka
kuwa wavumilivu kusubiriwa wataalamu wa sayansi ya bahari wafanyie kazi na
kutoa majibu wiki ijayo.
Hata hivyo Waziri Zungu aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukata
miti ovyo kwani ndio sababu kubwa ya maji ya bahari kujaa isivyo kawaida na
kuingia katika maeneo yao.
 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu (mwenye kofia kulia) akiwa ameambatana na
wataalamu wa mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) akitembelea ufukwe wa bahari jijini Dar es Salaam wakati
alipofika kutatua mgogoro uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya
wamiliki wa hoteli ya Wellworth na White Sands jijini Dar es Salaam
wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha mmonyoko wa udongo na hivyo maji
kujaa.
|
“Leo tunatazama mgogoro wa watu wawili kesho tutakuwa na wa
watu watano au sita, tupeni muda nimekuja hapa na mkurugenzi wa NEMC na
wataalamu wake kutazama na dawa ya changamoto tunayo kwa hiyo wiki ijayo
tutawaita na tutawaambia tulichofanya kuhakikusha kila mtu ana amani ndiyo kazi
ya Serikali,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka
aliwataka wawekezaji wote kufanya tathmni ya athari za mazingira (EIA) ili
kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima,
 |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mussa Azzan Zungu akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka apofika eneo la
ufukwe wa bahari jijini Dar es Salaam wakati alipofika kutatua mgogoro
uliotokana na changamoto za kimazingira kati ya wamiliki wa hoteli ya Wellworth
na White Sands jijini Dar es Salaam wakituhimiana kujenga ukuta unasababisha
mmonyoko wa udongo na hivyo maji kujaa.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Alisema kuwa binadamu tunaishi kwa kutegemeana kwenye
mazingira na ndiyo maana NEMC haitoi cheti hadi ifanyike tathmnini hiyo kubaini
madshara yanayoweza kutokea kwa wananchi kupitia uwekezaji unaofanyika.
“Natoa rai kwa wawekezaji wote wawe wa viwanda ama htoeli
katika fukwe zetu kufanya tathmni na kupitia tathmini hiyo tutapata maoni
kutoka kwa watu wanaokuzunguka kujua je uwekezaji wako unawaathiri vipi na kama
kuna athari ndogo tunajua namna ya kuzitatua ili kuepusha migioogoro,”
alisisitiza.
Akitoa maoni yake kuhusu changamoto hizo Mtaalamu wa Sayansi ya Bahari Rose Mtui alisema
kuwa suluhisho ni kuotesha mikoko ambayo inalunda fukwe zikibomoke kutokana na
mmomonyoko wa udongo.
Aliongeza kuwa uchimbaji
mchanga holela katika kingo za miti na uvuvi haramu unachangaia changamoto za
kimazingira katika fukwe za bahari kwani unaharibu matumbawe ambayo yakiharibika
mawimbi ya bahari higonga moja kwa moja na kwa kasi fukwe na hivyo maji kujaa
kupita kiasi.
|
No comments:
Post a Comment