Matokeo chanyA+ online




Wednesday, May 27, 2020

CCM YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA ILANI KATA YA UTENGULE, MAKAMBAKO

Na Amiri kilagalila,Njombe

Uongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe umesema umeridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho katika kata ya Utengule halmashauri ya mji wa Makambako,kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015-2020.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Njombe ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako HANANA MFIKWA wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo,ambapo amesema,miradi yote ikiwemo ya afya,miundombinu ya Barabara na umeme imetekelezwa kwa asilimia kubwa.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano afisa mtendaji wa kata ya Utengule MOSSES MWALONGO kwa niaba ya diwani amesema kuwa kata hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu msingi na Sekondari.

Naye diwani wa kata ya Utengule STEPHANO MGOBA amesema amefanikiwa kutekeleza miradi hiyo kutokana na kuwashirikisha wananchi na kueleza kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitano ametumia fedha zake binafsi zaidi ya milioni 20 kuwawezesha wananchi katika shughuli zao. Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo wameridhishwa na utendaji kazi wa diwani huyo kwa kipindi hicho cha miaka mitano.

No comments:

Post a Comment