Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akizungumza akipokea msaada wa vifaa kinga,vipeperushi,mabango na vifaa
vya kutoa elimu kwa umma kwa ajili ya watoa huduma za afya na waandishi
wa habari nchini
05/05/2020
Vifo vya watoto wachanga wenye umri wa chini ya siku 28 vimepungua
kutoka 25 kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwaka 2015/16 na kufikia
saba kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwezi Machi mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea msaada wa vifaa kinga, mabango,vipeperushi na vifaa vya kutoa elimu kwa Umma kuhusu ugonjwa wa Corona kutoka kwa Benki ya Absa Tanzania Ltd na Shirika la UNESCO.

Ummy Mwalimu ameishukuru UNESCO na bank ya Absa kwa msaada wao.Kutoka
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe na kulia kwa
Waziri ni Mkurugenzi wa Rasiliamali watu kutoka banki ya Absa Tanzania
Ltd. Patrick Foya
Waziri Ummy alisema kupungua kwa
vifo hivyo kumetokana na jitihada zilizofanywa na Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini hii ni
pamoja na kuboresha vituo vya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa
dawa, vifaa na vifaa tiba.
“Kwa namna ya kipekee niwapongeza na kuwashukuru wakunga wote hapa nchini kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kila siku ya kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano”,.

Mwakilishi
Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Tirso Dos Santos akikabidhi msaada wa
vifaa kinga pamoja na vifaa vya elimu kwa umma kwa ajili ya waandishi wa
habari
“Pamoja na
kuwa maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19)
yapo na watu wanaumwa ugonjwa huu, lakini tusisahau kuwa kina mama
wajawazito wanajifungua kila siku na wakunga wanaendelea kuwahudumia
kinamama hawa”, alisisitiza Waziri Ummy.
Waziri huyo aliwahakikishia wananchi kuwa pamoja na kuwa ugonjwa wa Corona upo huduma zingine zinaendelea kama kawaida katika vituo vituo vyote vya kutolea huduma za afya zikiwemo huduma za kliniki za akina mama wajawazito na watoto, upimaji wa magonjwa mbalimbali pamoja na upasuaji.

Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto-Idara
Kuu Afya Prof.Mabula Mchembe akiongea wakati wa kupokea msaada kutoka
UNESCO na Benki ya Absa Tanzania Ltd
“Ninawashukuru
wadau mliotoa vifaa hivi, ninawaomba wadau wengine waendelee kuiunga
mkono Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona ambao ni janga la
Dunia”,.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Mabula Mchembe alisema vifaa hivyo vitaboresha utoaji wa huduma za afya katika vituo vilivyopo Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Mabula Mchembe alisema vifaa hivyo vitaboresha utoaji wa huduma za afya katika vituo vilivyopo Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine nchini.
Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania, Tirso Dos Santos akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa Wizara ya Afya
Mkurugenzi
wa Rasiliamali watu kutoka banki ya Absa Tanzania Ltd. Patrick Foya
akiongea wakati wa kukabidi vifaa kinga ambavyo vitapelekwa kwenye vituo
vya kutolea huduma nchini
Na WAMJW – Dar es Salaam
“Ninawahakikishia wananchi pamoja na wadau mliotoa vifaa hivi kuwa vitatumiwa na wataalamu wetu katika kutoa huduma mbalimbali za matibabu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika vituo vyetu vya afya”, alisema Prof. Mchembe.
Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Rasiliamali watu wa benki ya Absa Tanzania Ltd. Patrick Foya alisema vifaa kinga walivyovitoa vyenye thamani ya milioni 20 ambavyo ni glovu, barakoa na vitakasa mikono vitawasaidia watoa huduma za afya wakati wanawahudumia wagonjwa.

No comments:
Post a Comment