|
Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye thamani ya
Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani ya sh. milioni 150
zilizotolewa na kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme nchini kwa ajili ya
kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona
(COVID- 19).
Waziri amepokea michango hiyo kwa
niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 4 Mei, 2020 katika Ofisi
ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo imetolewa na kampuni
Mufindi Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General Enterprises Co Ltd na
Poles (T) Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.
|
Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye thamani ya
Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Akizungumza wakati wa kupokea
michango hiyo Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa kuunga
mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa
COVID-19.
“Nawashukuru sana kwa niaba ya
Serikali na hii inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha kila Mtanzania
anakuwa ni sehemu ya mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri Mhagama.
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akizungumza
baada ya kupokea hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/=, zikiwa ni
mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya
ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa
Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Qwihaya General Enterpises Co.
Limited, Leonard Mahenda, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono
juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID
- 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma, Mai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Pia, Waziri Mhagama alitumia
fursa hiyo kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na Watanzania kuendelea
kushirikiana na Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali ili kuwezesha katika
kukabiliana na janga hilo.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wote
kuona umuhimu na kuguswa na janga hili kwa kuchangia kwa kadiri inavyofaa ili
kuendeleza uzalendo kwa hali ya kujali na kuonesha utayari ili kudumisha hali
ya utamaduni uliopo tangu awali wa umoja na mshikamano ,”alisema Waziri
Mhagama.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akipokea hundi ya
Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya
kuzalisha nguzo ya Mufindi Woodpoles Plant and Timber Limited, Salim Ahmed
Abeid, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za
mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano
hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4,
2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akipokea hundi ya
Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya POLES
(T) Limited, Salim Bisher Huwel, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga
mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu-
COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa
jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Aliwahakikishia wadau hao kuwa,
michango hiyo itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa imefika
katika eneo salama.
Awali, Waziri wa Nishati Dkt.
Medadi Kalemani aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa michanga waliyoitoa
kwa Serikali ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika kukabiliana na ugonjwa wa
COVID-19.
“Niwapongeze wakandarasi hawa kwa
kuonesha nia ya kushiriki katika mapambano haya na wito wangu kila anayeguswa
na janga hili ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini katika kuhudumia na
kusaidia katika kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi wengine waige, ”alisema
Dkt. Kalemani.
No comments:
Post a Comment