Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, tarehe 18 Mei 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Ili kukabiliana na uhaba wa masoko ya mazao ya kilimo serikali amezindua mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) ili kuwaunganisha wakulima na wanunuzi wa mazao yatokano na Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kuwa Sehemu
ya kwanza ni ya huduma za ugani ambayo itamsaidia mkulima kupata huduma
na ushauri wa kitaalamu kupitia simu yake ya kiganjani pasipo lazima ya
kukutana na Afisa ugani.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akionyesha kipeperushi wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, tarehe 18 Mei 2020. Wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba.
Amesema kuwa huduma hiyo imelenga
kutatua changamoto ya idadi ndogo ya maafisa ugani hapa nchini ambayo
imesababisha wakulima wengi kutokupata huduma za ugani.
Waziri Hasunga ameeleza kuwa Sehemu
ya pili ni ya huduma za masoko ambayo itamwezesha mkulima kupata
taarifa za masoko ikiwemo bei na mahali yalipo masoko kwa wakati husika.
Vilevile utamwezesha muuzaji kutangaza mazao yake sokoni, Mfumo huo pia utawawezesha wakulima na wataalam wa kilimo kuwasiliana kwa kutuma ujumbe kwa njia ya simu za viganjani.
Sehemu ya wataalamu mbalimbali wakifuatilia mkutano wa kazi wa Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizindua mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, tarehe 18 Mei 2020.
Waziri Hasunga amesema kuwa Mfumo huo umetayarishwa na wizara ya kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Halmashauri husika pamoja na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na jamii -ESRF.
Ameeleza kuwa mfumo huo utafanyiwa majaribio kuanzia tarehe 19 Mei, 2020 katika Wilaya za Bahi, Kongwa na Chamwino kwa muda wa Wiki moja.
Katika
majaribio hayo, jumla ya Maofisa ugani 35 na Wakulima 45 kutoka katika
kata mbili za Wilaya hizo watapata mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huu ambapo Washiriki watapata mafunzo yatakayowawezesha kuwafundisha wengine katika maeneo yao (TOT).
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, tarehe 18 Mei 2020.
Baada ya majaribio kufanikiwa, mfumo huo utapelekwa kwa wakulima wote nchini kwa ajili ya kuwawezesha kupata huduma za ugani.
Amesema kuwa ili kuweza kupata huduma kupitia M- kilimo mkulima anahitaji kulipia gharama ya ujumbe mfupi (sms) kwa kila huduma atakayohitaji ambapo Katika kipindi hiki cha majaribio (Piloting) gharama zitatolewa na Wizara.
Mfumo huo una faida
nyingi, lakini kubwa zaidi ni kufikisha huduma za ugani na za masoko
kwa wakulima na wafanya biashara hata wakati wa majanga ya milipuko ya
magojwa kama gonjwa la sasa hivi la COVID-19.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akifuatilia mkutano wa kazi wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kutoa huduma za masoko na huduma za ugani kwa njia ya mtandao (M-Kilimo) Jijini Dodoma, tarehe 18 Mei 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Aidha, kutokana na hali ya mlipuko wa ugonjwa wa CORONA, Wizara imejipanga kutekeleza zoezi hilo kwa kuzingatia tahadhali zote muhimu zinazotolewa na wataalam wa afya pamoja na viongozi nchini.
Waziri Hasunga pia ameeleza kuwa ili kuhakikisha kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani na soko la bidhaa unaleta tija kwa wananchi serikali imeamua kuanzisha aina mbili za masoko ambazo ni soko la awali na soko la upili.
Ili kufanikisha utekelezaji wa mifumo hiyo ni lazima kuwepo kwa vyama hai vya ushirika wa mazao (AMCOS) vilivyo sajiliwa kwa mujibu wa sheria; Kuwepo kwa maghala yaliyosajiliwa; kuainisha aina Mazao yanayohifadhika na kulinda ubora wake; na Elimu ya mfumo kutolewa kwa wananchi.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa M-Kilimo ni kutekeleza maagizo ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeaiagiza wananchi kuwa na uwezo wa kusafirisha mazao kadri wawezavyo bila kulipa kodi kwa mazao ambayo ni chini ya Tani 1 pamoja na Kupunguza usumbufu kwa wakulima.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) amesisitiza umuhimu wa soko la awali huku akiwaonya wakulima nchini kutochanganya mazao yao na uchafu ili kuongeza ukubwa wa mzigo.
No comments:
Post a Comment