Mkurugenzi wa Kampuni ya Vegrab Organic Farming LTD,Gladness Nyange,akizungumzia kilimo cha pilipili kichaa wakati wa uzinduzi wa zao hilo uliofanyika Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi, mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya Vegrab Organic Farming LTD kwa
kushirikiana na kampuni inayouza matrekta ya AGRI-COM wamezindua soko
la zao la pilipili kichaa litakaloweza kuwaongezea kipato wananchi wa
Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi,Mkoani
Singida.
Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo,Gladness Nyange alifafanua kwamba masoko ya zao la
pilipili kichaa ni makubwa sana isipokuwa kinachotakiwa ni uzalishaji
mkubwa na wenye ubora zaidi.
“Mimi
nina imani na zao hili nyie mnaliona hivi lakini ni zao ambalo
litatupeleka mbali sana kupitia juhudi ile tuliyoanzanayo tuendelee
nayo,kwani masoko ni makubwa sana lakini yanataka uzalishaji mkubwa
lakini pia wenye ubora.”alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Zao la pilipili baada ya kuvunwa.
Kwa
mujibu wa Nyange Mkoa wa Singida unaweza kuwa kituo kikubwa sana cha
uzalishaji wa zao la pilipili kichaa na siyo kwa Tanzania tu bali hata
kwa Afrika Mashariki na kwamba endapo wataweka jitihada wanaweza
kuongoza katika Afrika katika uzalishaji wa zao hilo.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa mazingira pamoja na ardhi iliyopo
katika Mkoa wa Singida inadhihirisha wazi kabisa kwamba pilipili
itakayozalishwa kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Singida itakuwa nzuri
kuliko inayotoka sehemu yeyote ile ya Tanzania na hata Afrika Mashariki.
Zao la pilipili baada ya kuvunwa.
Wakulima wa zao la pilipili wakiwa shambani.
Mkulima Mohemed Salehe, akizungumzia kilimo hicho.
Akizindua
mnada wa soko hilo la pilipili kichaa,Afisa ushirika wa Halmashauri ya
wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo alisema Kampuni inayonunua zao hilo
imesaini mkataba wa miaka mitatu na kwa msimu wa 2019/2020 kampuni hiyo
itanunua pilipili kichaa iliyoiva kwa bei ya shilingi 4,500/=kwa kilo
moja na shilingi 5,000/= kwa pilipili mbichi kwa kilo moja.
Aidha
Msemo alitoa sababu za soko la zao hilo kuzinduliwa katika Kata ya
Mtunduru kuwa ni kutokana na idadi kubwa iliyopo ya wakulima wa zao hilo
ambapo kati ya wakulima 159 waliolima pilipili kichaa Mkoani
Singida,110 ni wakulima kutoka wilaya ya Ikungi.
Mkulima Mwanaidi Iddi, akizungumzia kilimo hicho.
Na Jumbe Ismailly, Ikungi
Akimkaribisha kuzindua soko hilo,Mwenyekiuti wa Kipunda Amcos,Omari Nyuda huku akitumia kauli mbiu isemayo ongeza tija pilipili inalipa,alisisitiza juu ya uzalishaji bora wa zao hilo ili waweze kuendelea kupata fedha nyingi zaidi.
“Zao hili ambalo limekuwa na tija kwetu na kauli mbiu tunasema ongeza tija pilipili inalipa mradi na msimu umeshazinduliwa,kwa hiyo yetu ni mapesa,tupate pesa tuongeze uzalishaji tuongeze zao ubora zaidi tuweze kusonga mbele zaidi.”alifafanua Nyuda ambaye ni mwenyekiti wa Kipunda Amcos.
No comments:
Post a Comment