Awataka wakulima waendelee na kilimo katika kipindi hiki cha mpito
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa mazao mbalimbali ya
biashara wakiwemo wakulima wa ufuta nchini waendelee na kilimo na kwamba
suala la kushukuka kwa bei lililotokea kwenye msimu wa mwaka huu
lisiwakatishe tamaa kwani jambo hilo litakwisha.
Amesema
Serikali inaendelea kulifanyia kazi hilo na kwamba bei ya mazao nchini
itaimarika baada ya kuongezeka kwa ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao
nchini, ambapo wakulima watakuwa na masoko na uhakika na pia nchi
itauza bidhaa zitokanazo na mazao hayo na si malighafi.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Juni 24, 2020) wakati
akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Lindi alipokuwa katika ziara ya
kikazina aliwasihi wakulima kutoacha kulima.
“Kushuka
kwa bei ya ufuta kusiwakatishe tamaa na kuwafanya muache kulima kwa
sababu bei haijashuka kwa zao hilo tu bali na mazao mengine kama chai,
tumbaku, kahawa, chai na mazao mengine. Hali hii imetokana na mlipuko wa
ugonjwa wa COVID-19 ambao umeikumba dunia.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kadiri ugonjwa wa
COVID-19 unavyoendelea kupungua katika Mataifa mbalimbali duniani hali
bei ya mazao nayo itaimarika, hivyo wakulima waendelee kuwa na subira
katika kipindi hiki ambacho ni cha mpito.
Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kutoka ndani na nje ya
nchi waje wawekeze katika viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali kwa
sababu watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi pamoja na nishati
ya kutosha.
Alisema
moja ya msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ni kuboresha sekta ya kilimo ili iweze
kujitosheleza kwa chakula. “Suala la bei ya mazao linapangwa na wanunuzi
Serikali inasimamia tu.”
Pia,
Waziri Mkuu ameendelea kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa umoja na
mshikamano mkubwa waliompatia katika kipindi chote cha miaka mitano na
amewasisitiza waendelee na ushirikiano huo kwa ajili ya maendeleo ya
wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment