Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa
maelekezo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mary Makondo (wa tatu
kushoto), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt John Pima (Wa
kwanza kushoto) pamoja na Msajili Msaidizi wa Hati katika ofisi ya Ardhi
mkoa wa Arusha Juliana Ngonyani wakati akikagua masijala ya ardhi
alipokwenda kuzindua ofisi hiyo jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
amewataka Maafisa Ardhi nchini kuhakikisha wanawafuatilia wamiliki wa
ardhi ambao hati zao zimekamilika lakini hawataki kuzichukua ili
wazichukue katika kipindi cha siku tisini.
Lukuvi alisema hayo jana jijini Arusha wakati akizindua ofisi ya
ardhi ya mkoa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzindua ofisi za
ardhi katika mikoa mbalimbali nchini.
Waziri Lukuvi ambaye tayari amezindua ofisi za ardhi kwenye mikoa ya
Tanga na Manyara alisema, hivi karibuni Bunge lilipitisha sheria
inayotaka mmiliki wa ardhi aliyepimiwa eneo lake kuchukua hati katika
kipindi cha siku tisini na asipofanya hivyo utaratibu wa kumkata kodi ya
pango la ardhi utafanyika.
Baadhi
ya Watendaji wa sekta ya ardhi mkoa wa Arusha na wananchi wakimsikiliza
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo
pichani) alipokwenda kuzindua ofisi ya ardhi mkoa wa Arusha jana.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, kumekuwa na tabia ya baadhi ya
wamiliki wa ardhi kutojitokeza kuchukua hati za viwanja vyao kwa lengo
la kukwepa kulipa kodi ya pango la ardhi jambo alilolielezea kuwa
linamnyima fursa mbalimbali mmiliki sambamba na kuikosesha serikali
mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.
Alitolea mfano wa mkoa wa Arusha kuwa, pamoja na mkoa huo kuwa na
jumla ya viwanja 78,405 vilivyopimwa na hati zake kusajiliwa lakini ni
hati 29,000 pekee ndizo zilizochukuliwa na wamiliki wake na hivyo
kufanya hati 49,405 kutochukuliwa na kuikosesha serikali mapato ya
ardhi
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akikata utepe
kuzindua ofisi ya ardhi mkoa wa Arusha jana. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Arusha Idd Kimanta, wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary
Makondo na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Arusha Leo Komba.
‘’Ardhi ndiyo ulinzi wa rasilimali na inachangia kodi ya serikali kwa
hiyo wale wote wasiochukua hati wajitokeze katika kipindi cha siku
tisini, tunataka idadi ya viwanja vilivyopimwa na kuwekewa mawe ifanane
na hati zilizopo na wote waliopimiwa wakachukue baada ya hapo kama
hujachukua hati utaletewa invoice ya malipo’’ alisema Lukuvi.
Akizungumzia uanzishwaji ofisi za ardhi za mikoa, Lukuvi ambaye
alitoa hati 201 kwa wamiliki wa ardhi mkoa wa Arusha alisema, ofisi hizo
zimeanzishwa ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi na
kubainisha kuwa, sasa wananchi watapata huduma zote za ardhi kwenye
mikoa yao kama walivyokuwa wakipata Makao makuu ya Wizara na Ofsi za
ardhi za Kanda.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pamoja na
viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa mkoa wa
Arusha waliopatiwa hati za ardhi wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi ya
mkoa wa Arusha jana.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanti ameipongeza
wizara ya ardhi pamoja na mhe Rais John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa
kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za ardhi
za mikoa na kubainisha kuwa ofisi yake itatoa ushirikiano na kusaidia
masuala mbalimbali ya ofisi ya ardhi kwenye mkoa wake ili kufanikisha
azma ya serikali.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary
Makondo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe
Magufuli kwa kuwezesha utekelezaji jukumu la kusogeza huduma za sekta ya
ardhi karibu na wananchi kwa uanzishaji ofisi za ardhi za mikoa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Arusha jana. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo (Kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen (Kushoto). (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA
Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Arusha Komba alisema, tangu
kuanzishwa ofisi yake mwezi Machi mwaka huu tayari jumla ya hati 210
zimeandaliwa na 101 kutolewa kwa wamiki wake huku miamala 282 ikiwa
imefanyika na michoro 19 yenye viwanja 4,196 kuandaliwa sambamba na
Ramani 29 zenye viwanja 133 kuidhinishwa.
No comments:
Post a Comment