Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi akihutubia wakati akizindua Mradi wa Lishe Imara mkoani hapa jana unaoendeshwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Action Against Hunger. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Victolina Rudovick.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ameliomba Shirika lisilokuwa la
Kiserikali la Action Against Hunger kuanzisha kituo cha kutoa tiba kwa
watu wenye utapiamlo mkoani hapa.
Dk.
Nchimbi alitoa ombi hilo jana wakati akizindua Mradi wa Lishe Imara
mkoani hapa unaoendeshwa na shirika hilo mkoani Dodoma na sasa Singida.
Alisema
suala la Lishe halihitaji mgongano wa kifikra,ni suala lililonyooka
halina ama halina au ni mwelekeo mmoja tu na ni kweli na ni yakini.
Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi, akizungumzia umuhimu wa lishe kwenye uzinduzi huo.
"Nasema
hivyo ili kuonyesha kwamba mradi huu ni wa umuhimu sana kwa jamii na
ninapendekeza kituo hicho cha kutoa tiba kwa watu wenye utapiamlo
kijengwe hapa Singida." alisema Dk. Nchimbi.
Dk.
Nchimbi alisema kuna kila sababu ya kituo hicho kujengwa Singida kwa
kuwa kitakuwa jirani ya makao makuu ya nchi na kwamba eneo la kujenga
kituo hicho lipo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali kubwa ya kanda.
Mratibu wa mradi huo, Daud Tano akizungumzia lengo la mradi huo utakaofanyika katika mikoa ya Singida na Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Victolina Rudovick, akizungumza.
Afisa Lishe Mwandamizi Taasisi ya Chakula na Lishe, Maria Msangi akizungumza. Kulia ni Mratibu wa mradi huo, Daud Tano.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akizungumza.
Mratibu wa Mradi wa USAID Boresha Afya (Egpaf) Mkoa wa Singida, Dk.Nicholaus Njoka, akizungumza.
Akizungumzia
mradi huo Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk. Angelina Lutambi alisema mradi
huo wa Lishe Imara kwa Mkoa wa Singida unafaida kubwa,utawahusu wamama
wajawazito,wamama wanaonyonyesha na watoto chini ya umri wa miaka
mitano.
"Makundi
hayo mkuu wa mkoa umekuwa ukielekeza mara kwa mara kuhakikisha
tunapunguza vifo pamoja na mambo mengine hivyo ni lazima suala la lishe
likae sawa sawa na mama hatakuwa na changamoto yoyote ya kiafya na
atajifungua salama" alisema Lutambi.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wa Afya na Lishe wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mratibu wa Mradi huo Daud Tano alisema utalenga kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika Mkoa wa Singida na Dodoma.
Alisema
Mradi wa Lishe Imara unalengo Mahususi kutujengea Hospitali,Vituo vya
Afya pamoja na Zahanati jinsi ya kutambua, kutibu na kutoa huduma
stahiki ya masuala ya utapiamlo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi, akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Action Against Hunger.
Alisema
shabaha nyingine ya mradi huo ni kupunguza hali ya udumavu kwa watoto
wa miezi 0-59 kutoka asilimia 34 kwa 2015 hadi asilimia 28 ifikapo 2021
na kuzuia maambukizi mapya ya Utapiamlo mkali kwa watoto wa miezi 0-59
kwa asilimia 5 ifikapo 2021. Na kuongeza idadi ya watoto wenye umri wa
miezi 0-5 wanaonyonya maziwa ya mama pekee kutoka asilimia 41
(TNNS 2014) hadi kufikia asilimia 50 ifikapo 2021.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi
Na Dotto Mwaibale, Singida
Tano alisema Mradi huo watautekeleza katika Halmashauri nne ambazo ni Mpwapwa,Itigi,Mkalama pamoja na Iramba.
Mradi huo unalenga kuwafikia Vijana na watoto walio chini ya umri wa Miaka mitano na huduma zinazohusiana na Lishe hii ni pamoja na upimaji,matibabu pamoja na kuwajengea uwezo watoa huduma katika jamii.
No comments:
Post a Comment