Waziri wa Ardhi Nyunba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia bango linaloonesha
uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi mkoa wakati wa hafla fupi ya kuzindua ofisi
hiyo mkoa wa Tanga jana, Kulia kwa Waziri wa Ardhi ni Katibu Mkuu Mary
Makondo na wa tatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga martine Shigela.
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeeo ya Makazi William Lukuvi ameagiza kutolewa Hati za
umiliki wa ardhi ndani ya wiki pamoja pale mwananchi atakapokuwa
amekamilisha taratibu zote za umilikishwaji ardhi.
Aidha, ameagiza
wananchi kupatiwa hati zao za ardhi katika halmashauri waliolipia
gharama za kupatiwa hati ili kuondoa usumbufu pamoja na gharama kwa
mwananchi kufuatilia Hati kwenye Ofisi za Ardhi za mikoa.
Muonekano wa Ofisi mpya ya Ardhi
mkoa wa Tanga ambayo imezinduliwa rasmi jana na Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.
Lukuvi alitoa agizo hilo jana wakati akizindua ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga katika hafla fupi iliyofanyika jijini Tanga. Uzinduzi wa Ofisi hizo ulihudhuriwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo, Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shighela, Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Nghode, Katibu Tawala mkoa wa Tanga Judica Omari, Wakuu wa wilaya za mkoa wa Tanga pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za mkoa wa Tanga.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria
hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi mkoa wa Tanga uliofanywa na
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi jana.
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, wizara yake imekamilisha ndoto za
Rais John Pombe Magufuli za kuondoa usumbufu kwa wananchi kupata hati
za ardhi pamoja kufuata huduma za ardhi umbali mrefu na kutolea mfano
kuwa, mwananchi wa mkoa wa Tanga alilazimika kuifuata huduma ya ardhi
mkoani Kilimanajaro.
‘’Umekamilisha
taratibu zote za kupatiwa Hati hapa Tanga, unaambiwa ukachukue Moshi
ilipo ofisi ya Kanda, Rais ameliona hilo maana gharama za ufuatiliaji ni
kubwa kuliko hata ghrama ya kulipia hati yenyewe’’ alisema Lukuvi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika hafla fupi ya
kuzindua ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga jana. Wa pili kulia ni Waziri wa
Afya Ummy Mwalimu na wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine
Shigela na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akizungumza wakati wa halfa ya
uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga uliofanywa na Waziri wa Ardhi
William Lukuvi jana.
Aliwataka
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha pale hati za maeneo yao
zinapokamilika wamfuate Msajili Msaidizi wa Hati katika ofisi ya ardhi
ya mkoa kwa lengo la Msajili huyo wa Hati kwenda kuzikabidhi hati hizo
kwa wahusika kwenye halmashauri badala ya wananchi kuzifuta mkoani.
Kwa mujibu wa
Lukuvi, kumbukumbu zote za ardhi katika mkoa zilizokuwa ofisi za Kanda
nazo zimepelekwa mikoa husika na kutolea mfano kumbukumbu za mkoa wa
Tanga ambazo awali zilikuwa zikihifadhiwa Dar es salaam na baadaye
kuhamishiwa Moshi, Kilimanjaro sasa zimetunzwa Ofisi ya ardhi mkoa wa
Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine
Shighela akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa
wa Tanga uliofanywa na Waziri wa Ardhi William Lukuvi jana.Kulia kwa
mkuu wa mkoa ni Katibu Tawala mkoa wa Tanga Judica Omari.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimkabidhi mmoja wa wananchi wa mkoa
wa Tanga Hati ya umiliki ardhi jana wakati wa hafla fupi ya kuzindua
ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga jana. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga
Martine Shigela.
Alizitaja baadhi
ya kumbukumbu zilizo katika Ofisi ya Ardhi mkoa wa Tanga kuwa, ni pamoja
na Michoro zaidi ya 1,026, Ramani 5,400 pamoja na Hati 18,460 na
kusisistiza kuwa hati pamoja na nyaraka nyingine zimetunzwa vizuri na
wamiliki wake wanaweza kukopesheka bila matatizo yoyote.
Waziri Lukuvi
aliongeza kwa kusema, tangu kufunguliwa kwa ofisi mpya ya ardhi mkoa wa
Tanga tayari Hati zaidi ya 300 zimeandikwa na kusajiliwa kwenye mkoa na
kusisitiza kuwa, uanzishwaji ofisi za ardhi kwenye mikoa siyo tu
utaondoa usumbufu wa kufuatilia hati bali utapunguza pia migogoro ya
ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kulia) Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine
Shigela (wa pili kulia), Katibu Tawala mkoa wa Tanga Judica Omari
(aliyevaa miwani) na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Mary Makondo (kushoto)
wakiangalia samani za ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga iliyozinduliwa jana
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na
wananchi wa mkoa wa Tanga waliokabidhiwa Hati zao za umiliki wa ardhi
wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga jana.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema, jitihada zilizofanywa na serikali kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa zina lengo la kumpunguzia mwananchi usumbufu wa kufuata huduma ya sekta hiyo umbali mrefu ambapo huduma hiyo ilikuwa ikipatikana ofisi za kanda na kila kanda ilikuwa ikihudumia mikoa mitatu au zaifi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Makatibu Tawala wa wilaya za mkoa wa Tanga (waliosimama mbele)
wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga jana.
Mbunge wa Jimbo la Lushoto Shabani
Shekilindi (Bosnia) akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi ofisi
ya ardhi mkoa wa Tanga jana.
Alisema, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inakusudia ardhi yote nchini ipangwe, kupimwa na kumilikishwa ili wananchi waweze kupewa miliki huku hatua hiyo ikilenga pia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa
Tanga Tumaini Gwakisa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ofisi yake
wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya ardhi mkoa wa Tanga uliofanywa
na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
jana (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI).
Na Munir Shemweta, WANMM TANGA
Naye Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Martine Shigela amewataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa
wake kuhakikisha wanaitumia vyema fursa ya uwepo ofisi za ardhi za mkoa
katika kuwawezesha waanchi kupata hati zao kwenye eneo la halmashauri
husika badala ya kwenda mkoani sambamba na kutatua migogoro ya ardhi kwa
kutumia wataalamu waliopo ofisi ya ardhi ya mkoa.
No comments:
Post a Comment