Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Royal Group Ndugu Hassan Mohammed Raza Kushoto
akimuonyesha Ramani ya Hoteli Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif alipofanya ziara fupi.
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezishauri Kampuni za
Uwekezaji katika Sekta ya Biashara kuangalia uwezekano wa Kujenga
Hoteli ya Kitalii katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa lengo la kutoa
huduma kwa wasafiri na hata Wananchi wanaotumia Uwanja huo.
Alisema
mfumo wa huduma za Mahoteli unaokuwepo katika Viwanja mbali mbali vya
Ndege Duniani hulenga kuwaondoshea usumbufu Wasafiri wa Anga kuzitafuta
huduma hizo maeneo ya Mijini kwa vile baadhi ya Viwanja hivyo huwepo
Ng’ambo ya Miji.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo alipofanya ziara fupi ya kukagua
Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Golden Tulip
Airport Hotel iliyopo pembezoni mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Aman Karume ulio chini ya Kampuni ya Royal Group.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi zake za Uwekezaji ina
nia ya kuona fursa ya ujenzi wa Hoteli ya Kitalii katika Uwanja wa
Ndege wa Pemba inachangamkiwa na Wafanyabiashara wenye uwezo kwa
kuanzisha Mradi huo muhimu unaoweza kutoa huduma sambamba na ajira kwa
Vijana.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi mzima wa Kampuni ya
Royal Group kwa uamuzi wake wa kuanzisha Mradi huo Mkubwa utakaosaidia
kuongeza Pato la Taifa, huduma kwa Wasafiri na kwa upande mwengine Ajira
kwa Wananchi Wazalendo.
Mapema
akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika maeneo mbali mbali
ya Jengo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Royal Group Ndugu
Hassan Mohammed Raza alisema ujenzi huo unaotarajiwa kuchukuwa Miezi 16
utakamilika ifikapo Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Ndugu
Hassan alisema ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na Vyumba 62 vya
kulala, eneo la kuegesha magari 150 kwa wakati Mmoja linatarajiwa
kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 7.5 sawa na fedha za
Kitanzania Zaidi ya shilingi Bilioni 17.1.
Mkurugenzi
Hassan alimueleza Balozi Seif kwamba pamoja na mambo mengine Uongozi wa
Royal group umezingatia huduma za Michezo kwa kuweka Bwawa maalum la
kuogelea pamoja na sehemu za mazoezi kwa wale wasafiri wanamichezo.
Alisema
Mradi huo utakapokamilika utatoa huduma kwa Wasafiri wa Anga wanaotumia
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa kuzingatia umuhimu wa
usalama wa Abiria unaokwenda sambamba na vile vigezo vya Viwanja vya
Ndege vya Kimataifa.
Naye
Meneja wa Operesheni wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar
{AAKIA} Nd. Haji Haji alisema vifaa Maalum vitawekwa katika Hoteli hiyo
vitakavyosimamiwa na Watendaji wa Taasisi zote zinazohusika na masuala
ya Uwanja wa Ndege katika kuona Msafiri anapata huduma zinazostahiki.
Nd.
Haji alisema usafiri wa Mabasi utawekwa kwa ajili ya kuwahudumia abiria
wanaokuwemo ndani ya Hoteli hiyo na kuwafikisha kwenye mlango na ndege
wanazosafiria.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/07/2020.
No comments:
Post a Comment