Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (Tamisemi)
Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha
kuzalisha vifaa vy umeme katika Kiwanda cha AfriCab jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikioa na Tawala za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo amesema kuwa fedha zinazoelekezawa katika Miradi ya Miundombinu ya ujenzi katika Halmashauri na Mikoa kuhakikisha wananunua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Jafo
ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha
vifaa vya Umme cha Africab kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam ,
amesema kuwa kulinda viwanda vya ndani ni kuhakikisha bidhaa
zinazozalishwa zinapata soko la kutosha ikiwa pamoja na kulinda ajira
zinazotolewa kwa wananchi katika viwanda hivyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza kuhusiana na ziara ya
Waziri Jaffo katika kiwanda cha African kilichopo Kurasini Jijini Dar es
Salaam.
Amesema
Africab imewekeza katika vifaa vya umeme ambapo vinakidhi viwango hivyo
hakuna sababau ya kununua biadhaa za nje wakati bidhaa za ndani zina
vwango kuliko bidhaa za nje ya nchi.
Jafo
amesema kuwa watanzania kwa pamoja wakinunua bidhaa zinazozalishwa
katika viwanda vya ndani kutafanya wanaoagiza biadhaa hizo na kuanza
kuagiza katika viwanda vya ndani hali ambayo itafanya viwanda kuongeza
uzalishaji pamoja na ajira kuongezaka kwa wazawa.
Mkurugenzi wa Africab Mansour Moizz akimpa maelezo namna wanavyozalisha bidhaa mbalimbali ndani ya kiwanda.
"Tanzania
sio nchi kuwa jalala kwa bidhaa zisizo na ubora na wananchi wanatakiwa
kuwa walinzi wa bidhaa zinazolishwa katika viwanda vya ndani ,ulinzi
wa bidhaa za ndani sio kutumia bunduki bali ni kukunua kuthamini bichaa
zinazalishwa katika viwanda vya ndani"amesema Jaffo.
Aidha
amesema Africab wameajiriri wafanyakazi 400 ambapo ni watanzania hivyo
kuacha kununua bidhaa katika kiwanda hicho ni kutaka kupoteza ajira za
wafanyakazi hao.
Afisa
Masoko wa Africab David Tarimo akizungumza kuhusiana ziara ya Waziri
Jaffo namna alipowapa moyo ya kuzalisha vifaa vya umeme.
Amesema
kuwa nchi kuingia uchumi wa kati ni pamoja na viwanda vilivyojengwa na
vinavyoendelea kujengwa hivyo bidhaa zinazozalishwa ndani zitumike
katika ujenzi wa vitu mbalimbali.
Nae
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amesema kuwa kauli ya Waziri wa
Tamisemi kilichobaki ni utekelezaji tu katika miradi kwa wilaya ya
Temeke kununua bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani.
Gondwe amesema kuwa Temeke imepata bahati ya kuwa na Kiwanda kikubwa cha vifaa vya umeme na vina ubora.
Afisa Masoko Mkuu wa AfriCab Deo Rwakagera akiomuonesha Waziri Jaffo bidhaa za vifaa vya umeme zilizozalishwa na AfriCab.
Afisa
wa Masoko wa Kiwanda cha Africab, David Tarimo amesema kuwa wameanza
uzalishaji miaka 19 walianza na kutengeneza nyaya za umeme lakini sasa
wamekwenda mbali wanategeneza hadi mitambo ya kupoozea umeme.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa kiwanda cha Africab wakiwa katika majukumu ya kazi katika kiwanda hicho.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Amesema kuwa ziara ya Waziri Jaffo inafungua milango ya kuafanya kuendelea kuzalisha zaidi kwa kupanua masoko
Tarimo
amesema kuwa bidhaa hizo wanauza Afrika Kusini, Malawi, Zambia pamoja
na Rwanda hivyo soko linahitajika zaidi kwa kwa uzalishaji unaanza wa
kebo za umeme.
No comments:
Post a Comment