Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa
Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameanza ziara ya kukagua na kufuatilia
ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kata zote za Tarafa ya Mihambwe
ambapo ameridhishwa na ujenzi na ukamilifu wa miradi ya ujenzi ya nyumba
ya Mwalimu pamoja na vyoo shule ya Msingi Mpunda iliyopo Kijiji cha
Mpunda kata ya Michenjele.
Hayo yamejidhihirisha kwenye ziara
hiyo aliyoifanya Gavana Shilatu ambapo amefurahishwa na ubora wa miradi
hiyo ambayo pia imekamilika kwa wakati.
“Kazi kubwa imefanyika,
ni ngumu kuamini leo hii kwa mara ya kwanza Kijiji cha Mpunda wanakuwa
na nyumba ya kisasa ya kuishi ya Mwalimu pamoja na vyoo vya kisasa vya
Wanafunzi na Walimu. Shukrani kwa Rais Magufuli kwa kutupatia fedha
takribani Tsh. Milioni 37. Nawasisitiza kuitunza miradi hii idumu kwa
manufaa ya nyakati zote.” Alisisitiza Gavana Shilatu.
Nae Mwalimu Seleman Seleman ameshindwa kuzuia hisia zake kwa Rais Magufuli ambaye amewezeshwa ukamilifu wa miradi hiyo.
“Miradi
yote ya nyumba na vyoo imekamilika kwa asilimia 100, kiukweli
tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kutujali Watumishi hususani Waalimu
kwa kutoa fedha za kujengea nyumba hii.” Alisema Mwalimu Seleman.
Mradi
wa nyumba ya Mwalimu umegharimu Tsh. Milioni 33.5 na ukarabati wa vyoo
kwa Tsh. 3.5 na miradi yote imeshakamilika kwa asilimia 100 tayari kwa
matumizi.
No comments:
Post a Comment