Na.WAMJW-Dar es Salaam
Wamiliki
wa Maabara Binafsi za Afya wameelekezwa kufuata sheria na taratibu
zinazosimamia uendeshwaji wa Maabara hizo ili wagonjwa wapate majibu
sahihi yatakayopelekea huduma bora za matibabu kwa wagonjwa.
Hayo
yamebainishwa na Msajili wa Bodi ya Maabara Binafsi za Afya nchini
Bw. Dominic Fwiling’afu wakati wa ukaguzi wa Maabara Binafsi za Afya
katika Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam.
Msajili
wa Maabara binafsi za Afya Bw. Dominic Fwiling'afu akitoa elimu kwa
mtaalamu wa maabara wakati wa ukaguzi wa maabara jijini Dar es Salaam
Bw.
Fwiling’afu amesema ukaguzi huo umefanyika kwa lengo la kuangalia hali
ya utoaji wa huduma za Maabara Mkoani Dar es Salaam lengo ikiwa ni
kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za Maabara ambazo
zitawasaidia matabibu kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
“Katika
ukaguzi wetu tumepita katika Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam,
tumefanya ukaguzi, tumetoa elimu , ushauri na maelekezo magine ili
kuboresha huduma. Lakini pia kuna baadhi ya Maabara tumelazimika
kuzifungia kwani zimekua zikiendeshwa kwa kukiuka sheria Na. 10 ya Mwaka
1997 Pamoja na kuhatarisha maisha ya watanzania wanaofika kupata huduma
katika vituo hivyo” Alisema Bw. Fwiling’afu
Amesema
Pamoja na kuzifungia baadhi ya Maabara ambazo zimekua zikiendeshwa kwa
kukiuka sheria zipo Maabara ambazo zimepongezwa kwa kutoa huduma bora
kwa kufuata sheria na miongozo na hivyo kupelekea wananchi kupata huduma
bora za Maabara.
Kwa upande wake Mratibu wa
huduma za Maabara Wilaya ya Ilala Petrobas Hassan ameishukuru Wizara ya
Afya kwa kufanya ukaguzi huo katika jiji la Dar es Salaam kwa kuwa kuna
maabara nyingi na zinahitaji kujengewa uwezo ili zitoe huduma bora kwa
wananchi.
“Naishukuru sana Wizara ya Afya
kupitia Bodi ya Maabara Binafsi za Afya, kwa kuja kufanya ukaguzi huu,
mimi kama maratibu nimefarijika sana maana ninaowasimamia wamepata
elimu, ushauri Pamoja na maelekezo mengine yanayolenga kuboresha huduma
hivyo nashauri ukaguzi huu ufanyike mara kwa mara ili kuendelea
kuboresha huduma” Alisema Bw. Petrobas
Mtaalam
wa maabara kutoka kituo cha Ibrahim Haji cha jijini Dar es Salaam Bw
Deogratious ameishukuru Wizara ya Afya kwa kufanya ukaguzi na kutoa
mafunzo kwa wataalamu wa Maabara jambo ambalo limewaongezea ujuzi na
maarifa katika kufanya kazi zao za kila siku na kuhakikisha wananchi
wanapata majibu sahihi kwa wakati ili kupata tiba bora.
No comments:
Post a Comment