Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Ali Bashiru amewataka wote waliotia nia kugombea ubunge
kubaki kwenye majimbo yao kusubiri majina yatakayopitishwa na Halmashauri Kuu
ya chama hicho inayokaa Dodoma Agosti 20, 2020.
Dk. Bashiru amesema inabidi wabaki kwenye majimbo yao
ili iwe rahisi kwa watakaopitishwa kugombea, kwenda kuchukua fomu, kutafuta
wadhamini na kurejesha fomu ili Agosti 25 mwaka huu wazirejeshe Tume ya Taifa
ya Uchaguzi kwa ajili ya uteuzi.
Ameyazungumza leo baada ya kuzindua Kituo cha CCM CHA Mawasiliano ya Habari za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ambao kampeni zake zinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema kuwa leo kimekaa kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri
Kuu ya Taifa, kuandaa taarifa ya wagombea itakayopelekwa kesho katika kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuchuja majina kwa mujibu wa katiba
ya chama hicho na hatimaye kuyapeleka Halmashauri Kuu Agosti 20 itakayoteua
jina moja la mgombea kwa kila jimbo na wagombea wa viti maalumu.
“Kazi ya Sekretarieti siyo kufanya uteuzi bali ni kuandaa
nyaraka, kufanya uchambuzi taarifa za vikao vya wilaya na mikoa za watia nia
ubunge na wa viti maalumu ngazi ya Taifa, tunachambua na kuandaa mapendekezo na
kuvipeleka Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na hatimaye
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa aijili ya uteuzi.” Amesema na kuongeza
kuwa…
“Tunarajia sifa za chama chetu ndiyo msingi mkubwa, na chama
chetu kwa sifa zake tutakuwa pia na viongozi wenye sifa hizo, kwa hiyo sifa za
viongozi wanaotakiwa zipo kwenye Katiba na kanuni za uteuzi , mwadilifu, mchapakazi,
jasiri, mzalendo, msikivu kwa anaowaongoza, mwenye nidhamu ya kutii maelekezo
ya vikao wa chama.”
Amesema kuwa anatatarajia katika waliotia nia kugombea zaidi 10,000, kati yao watapata wagombea bora, kwa sababu ya kipimo cha chama
ni kuwa na hazina ya viongozi, ni idadi
ya waliotia nia na kwamba mchakato
umekuwa wazi kwa nchi nzima, kwenye urais, ubunge na udiwani. Kuhusu
wawakilishi utaratibu wake utafanyika baadaye kwani ratiba ya uchaguzi na kampeni imekuwa tofauti
kwa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment