Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Bashiru akiwasiliana na
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, kwa simu iliyopigwa kwenye kompyuta
mpakato (Laptop) ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano
cha CCM kuhusu Habari za Uchaguzi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete,
jijini Dodoma leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Dk.
Bashiru akiangalia picha za wagombea urais kupitia CCM zilizopambwa
upenuni mwa kituo hicho. Wagombea hao ni Dk. John Magufuli anayewania
urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza Samia Suluhu Hassan
pamoja na Mgombea urais Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi.
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, Gabriel Athuman akiangalia mpangilio ulivyo ndani ya kituo hicho.
Afisa
Tehama wa CCM, Magoti Wambura akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM, Dk.
Bashiru, jinsi wanavyowasiliana na viongozi, wanachama na umma kupitia
kwenye kompyuta mpakato wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha habari za
uchaguzi.
Baadhi ya watumishi wa kituo hicho
Dk. Bashiru akiangalia kituo hicho wakati akipata maelezo kutoka kwa Afisa Tehama, Wambura (kushoto). Kulia ni Gabriel Athuman.
Afisa
Tehama wa CCM, akitoa maelezo kwa Dk. Bashiru jinsi kituo hicho
kitakavyopokea taarifa mbalimbaliza za uchaguzi kupitia kituo hicho.
Dk
Bashiru akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambapo alisema
kuwa hivi sasa kituo hicho kitakuwa kinakusanya taarifa mbalimbali za
uchaguzi kutoka kwa viongozi wa CCM, Wanachama na Umma na baada ya
uchaguzi kazi yake kubwa itakuwa kukusanya Taarifa za Utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi.
Dk. Bashiru akizungumza na wanahabari kuhusu kazi ya kituo hicho.
Mtumishi wa kituo hicho, Debora Kiyuga akiwa tayari ameanza kazi ya mawasiliano
Neema Mfugale akiweka mambo sawa
Zuhura Hassan akiwa kazini
Baadhi ya watumishi wakiwa kazini kituoni hapo
No comments:
Post a Comment