Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives (ESTL), Joshua Ntandu, akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wadau mbalimbali wa Kata ya Kinyagigi katika Wilaya ya Singida Vijijini kwa ajili ya kuunda kamati za vijiji za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Veronika Mure na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kinyagigi, Nives Mapunda.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Veronika Mure, akizungumzia majukumu ya Mtakuwwa.
Shirikisho
lisilo la kiserikali la Empower Society Transform Lives
(ESTL)limewakutanisha wadau mbalimbali wa Kata ya Kinyagigi katika
Wilaya ya Singida Vijijini kwa ajili ya kuunda kamati za vijiji za
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Wadau
waliokutanishwa na shirika hilo ili kupata mafunzo ya kupinga ukatili
wa kijinsia na kuunda kamati hiyo ni wakunga wa jadi, walimu wa afya
mashuleni, wahudumu wa afya ngazi ya jamii, waganga wa tiba asilia,
mangariba na watu wenye mahitaji maalumu.
Wadau wakipitia mwongozo wa Mtakuwwa.
Kikao
hicho kilicho keti mwishoni mwa wiki katika kata hiyo kililenga kuunda
kamati za vijiji zitakazokuwa zikifuatilia vitendo vya ukatili katika
wilaya hiyo pamoja na kupitia mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili
dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA 2017/18 hadi 2021/22.
Akizungumza
katika kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Joshua Ntandu
alisema shughuli hiyo inafanyika kwa ufadhili wa Ubalozi wa Finland Dar
es Salaam kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya
ya Singida vijijini kwa kutekeleza mradi huo katika Kata tano ambazo ni
Maghojoa, Mwasauya, Merya, Munghunga na Kinyagigi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kinyagigi, Nives Mapunda, (katikati) akizungumza katika kikao hicho.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyagigi, Hamisi Mohamed, akizungumza katika kikao hicho.
Alisema
shughuli ambazo kamati hiyo itazifanya kwa kushirikiana na shirika hilo
ni kukutana na kina mama wanaohudhuria kliniki na kuwapa mafunzo, kutoa
mafunzo kwa viongozi wa dini, vijana walio nje ya shule,wanafunzi
mashuleni na kuimarisha klabu za wanafunzi (KLABU JUU)
Alitaja
shughuli nyingine ni kuandaa midahalo ya wazi ya kujadili namna ya
kutokomeza mila potofu na kufanya mikutano ya hadhara.
Mwakilishi wa vijana wa kata hiyo, Alfred Mohamed, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kwa
upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Veronika Mure
alisema majukumu ya kamati hiyo nikuhakikisha utekelezaji wa mpango kazi
huo na shughuli za hutoaji huduma kwa makundi yaliyo katika mazingira
hatarishi unaendana na mikataba ya Kikanda na Kimataifa ya haki na
ustawi wa Wanawake na Watoto pamoja na Sera, Sheria na Miongozo ya
Serikali.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mitula, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Washiriki
wa kikao hicho walisema vitendo vya ukeketaji na matukio ya ukatili wa
kijinsia bado ni changamoto na kwamba maovu hayo hufanyika kwa siri
kubwa.
“Matukio
ya vitendo vya ukeketaji na ukatili wa kijinsia bado vinafanyika na
kibaya zaidi watuhumiwa wakikamatwa na kufikishwa polisi au mahakamani
huachiwa hivyo kuleta sintofahamu miongoni mwa jamii" alisema mmoja wa
wajumbe hao Jackline Alute.
Majadiliano yakifanyika.
Kiongozi wa Dini ya Kikristo, Emanuely Ng'eni, akizungumza kwenye kikao hicho.
Alute
alisema suala la ukeketaji, mimba na ndoa za umri mdogo yamekuwa ni
matukio ya kawaida na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa hata baada ya
kumbaini mtuhumiwa walalamikaji na ndugu wa mtuhumiwa hukutana na
kuyamaliza kiaina.
Katika
kikao hicho wajumbe hao walijifunza mbinu za kuibua vitendo vya ukatili
wa kijinsia na jinsi ya utoaji wa taarifa kwa vyombo husika kwa
kushirikiana na ESTL.
Na Dotto Mwaibale, Singida
Washiriki hao walipata fursa ya kukaa katika makundi na kutengeneza mpango kazi utakaowaongoza katika kutekeleza majukumu yao dhidi ya vita ya matukio ya ukatili wa kijinsia na ukeketaji ambapo kila baada ya miezi mitatu watakuwa wakifanya kikao cha tathmini.
“Lengo la mpango kazi wetu huu ni kutusaidia kuanza kuibua matukio yote ya ukatili, kuhamasisha jamii kuacha kufanya vitendo hivyo na kufanya ufuatiliaji na hatimaye kutoa taarifa kwa MTAKUWWA na kwenye mfumo wa Tehama uliobuniwa na ESTL ili kutoa taarifa za matukio ya ukatili kwa kutumia namba 0710567003, “ alisema Alfred Mohamed.
No comments:
Post a Comment