Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge akizungumza wakati wa zoezi
la uchangiaji damu lililofanyika katika Hospitali ya Ebrahim Haji kwa
kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama. kushoto ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji akitoa maelezo wakati
wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Jumuiya ya Khoja Shia
Ithnasheri kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na
Hospitali ya Ebrahim Haji.
Sehemu
ya watu waliojitokeza katika wakati wa zoezi la uchangiaji damu
lililoendeshwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kushirikiana na
Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji.
Sheikh
Sayed Idairous kutoka katika Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri akitoa
maelezo wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Jumuiya ya
Khoja Shia Ithnasheri kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama
na Hospitali ya Ebrahim Haji
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Abubakar Kunenge ameipongeza Jumuiya ya
Khoja Shia kupitia programu yake ya “Husayni Blood Drive” kwa
kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa
wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji. Zoezi hilo la uchangiaji
damu limefanyika katika Hospitali ya Ebrahim Haji iliyopo jijini Dar es
Sala ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa
Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain lakini pia ikiwa ni kuendeleza
utamaduni wa kujitolea kwa jamii ambao ni msingi mkuu wa ujumbe wa Imam
Hussain.
Akizungumza
katika zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa amepongeza jumuiya ya Khoja Shia
Ithnasheri kwa tukio hilo lenye upendo kwa kuwa linaenda kuokoa maisha
ya watu. “Nimeambiwa kuwa zoezi hili limefanyika kwa zaidi ya miaka 15
na kukusanya zaidi ya lita 5000 za damu ambazo zimesaidia kuokoa maisha
ya watanzania wengi jambo ambalo ni lenye upendo mwingi kwani watu hawa
wanachangia damu bila kujali inakwenda kumsaidia nani” alisema Mkuu wa
Mkoa.
Mkuu
wa Mkoa amesema watu wengi wanapenda kutoa msaada pale ambapo wana
uhakika wa kupata shukrani na hivo kutoa msaada kwa watu wanaowajua au
kuwaona lakini Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri imefanya sadaka
iliyobora kwa kutoa damu kwa watu wasiowajua ambao hawatopata hata
nafasi ya kuwashukuru na hiyo ndiyo sadaka bora kwa mujibu wa vitabu vya
dini.
Mkuu
wa Mkoa pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji kwa kushiriki katika matukio mengi ya
kitaifa ikiwemo kutoa nyumba yake binafsi ili kutumika kama kituo cha
kuhudumia wagonjwa waliopata maambukizi ya Corona.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri, Azim Dewji
alisema kuwa jumuiya hiyo imekua ikishiriki katika mambo mengi ya
kijamii ambapo mapema mwaka huu, Jumuiya hiyo hiyo ilitumia siku 45
kujenga wodi mpya yenye vitanda 60 katika Hospitali ya Ebrahim Haji ili
kusaidia wagonjwa waliopata maambuzi ya Corona.
Hata
hivo kutokana na kupungua kwa maambukizi ya Corona nchini, wodi hiyo
sasa itatumika kuhudumia akina mama na watoto. Pamoja na hilo kila
Jumamosi hospitali hiyo hutoa huduma bure za matibabu kwa watoto yatima
na wale wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni sehemu ya mchango
wake kwa jamii.
Nae
Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu Kanda ya Mashariki, Judith Goshashy
ameipongeza Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri kwa kuwa wachangiaji wazuri
wa damu kwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) tangu walipoanza
kushirikiana nao mnamo mwaka 2008. “Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita
tumekua tukipokea wastani wa wachangiaji damu 440 kila mwaka kutoka
katika Jumuiya hii jambo ambalo ni la kupongezwa sana ukizingatia huwa
wanajitolea damu mara 2 kwa mwaka” alisema Judith.
Sheikh
Sayed Idairous ambae ni mmoja wa viongozi wa dini kutoka katika Jumuiya
ya Khoja Shia Ithnasheri, alisema kuwa wajibu wa viongozi wa dini
katika nchi ni kujenga undugu bila kujali itikadi za dini wala kabila na
hivyo wao wamechagua kufanya zoezi hilo la uchangiaji damu ambalo
linakwenda kusaidia watu bila kujali itikadi zao. “ Damu hii inayotolewa
hapa haitouliza dini ya mtu wala kabila lake bali itakwenda kusaidia
kukoa maisha ya watu na huo ndio wajibu wetu” alisema Sheikh Sayed.
Pamoja
na zoezi la kuchangia damu,Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri pia
hushiriki katika shughuli nyingine za kijamii ikiwemo utoaji wa maji
safi, uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho, uchunguzi wa saratani
zinazoathiri wanawake ikiwemo saratani ya matiti na mlango wa kizazi.
“Huduma hizi zimekua zikifanyika kwa takribani miaka 5 sasa na hutolewa
bila malipo kwa wagonjwa wote wanaojitokeza” alisema Dr. Alihussein
Molloo ambae ni mwanajumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri na Mkurugenzi wa
Hospitali ya Ebrahim Haji.
No comments:
Post a Comment