Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akizungumza jambo alipotembelea kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro
Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kutengeneza sera itayowezesha wanafunzi Mil 10
hadi Mil 20 wa shule za msingi na Sekondari wanaoanza masomo yao
kutumia viatu vitakavyozalishwa na Kampuni ya bidhaa za Ngozi ya
Kilimanjaro iliyopo mjini Moshi .
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega wakati ya ziara ya siku moja mkoani Kilimanjaro ambapo ametembelea mradi wa ujenzi wa viwanda vya kuchakata bidhaa za ngozi vilivyopo chini ya kampuni ya Kilimanjaro Leather Industries Co Ltd.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivi ,Abdalah Ulega akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bidhaa za ngozi ya Kilimanjaro Mhandisi Masud Omari wakat wa ziara yake ya siku moja kiwandani hapo.
Akizungumza
mara baada ya kujionea hatua za ujenzi zilipofikia Naibu Waziri Ulega
alisema katika kuunga Mkono Jitihada za Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dk John Joseph Pombe Magufuli za kuipeleka Tanzania
kwenye uchumi wa viwanda, Mfuko Wa PSSSF umewekeza katika Mradi wa
ujenzi wa Kiwanda kipya cha Bidhaa za Ngozi Mkoani Kilimanjaro .
“Wito
wangu tu ni kwamba taasisi za serikali ,ni muhimu sana zikanunua bidhaa
zetu sisi wenyewe tunazozalisha hapa sisi wenyewe hapa nyumbani ,kwa
mfano watu wengi hawajaamini kama vitu vinavyotengenezwa na
wajasiliamali wadogo wadogo na viwanda vyetu kama kweli ni ngozi
.álisema Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.
“Tunalo
tatizo la bidhaa hizi za plastiki yaliyokarabatiwa karabatiwa
,yameingia kwa wingi sana ,yamefanya hata wajasilia mali wetu hapa zile
bidhaa wanazotengeneza sio ngozi ,lakini zile ni ngozi na watanzania
tuamini kwamba zile ni ngozi.”aliongeza Ulega .
Alisema serikali inakusudia kuanza na watoto katika
mashule ya msingi na Sekondari baada ya kukubaliana na watungaji sera
na viongozi katika wizara mbalimbali ambapo watoto kati ya Mil 10 na 20
watapata viatu
Moja ya majengo ya kiwanda hicho yaliyojengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hiki Mhandisi Masud Omar amesema Kampuni hiyo pamoja na kampuni za Italia ,TMC na ITALPROGETTI wapo kwenye taratibu za mwisho za kuanza kazi ya kusimika mitambo na kwamba janga la virusi vya Corona vimechangia kuchelewa kwa kazi hiyo.
“Ili
kutekeleza agizo la Serikali, Kampuni ijulikanayo kwa jina la “Karanga
Leather Industries Co Ltd” (KLICL) ilianzishwa mnamo tarehe 30 Mei, 2017
kwa lengo la kuanzisha mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo
la Gereza la Karanga, Moshi, Kilimanjaro kwa lengo la kuboresha kiwanda
cha ngozi kilichopo na baadae kujenga kiwanda kipya cha kisasa cha
utengeneaji wa ngozi na bidhaa zake. “alisema Mhandisi Omari .
Sehemu ya mashine zilizofika kwa ajili ya kusimikwa katika kiwanda hicho.
Mhandisi
Omari alisema kampuni hiyo ilianzishwa kwa ubia kati ya uliokuwa Mfuko
wa Pensheni wa PPF, ambao kwa sasa majukumu yake yamechukuliwa na PSSSF
pamoja na Jeshi la Magereza kupitia kampuni yake ya Prisons Corporation
Sole.
“Hatua
ya kwanza (LOT 1) ya utekelezaji wa mradi inayohusisha ujenzi wa
kiwanda cha viatu yaani ujenzi wa jengo ya Ukataji na ushonaji,
umaliziaji, ghala na nyumba ya umeme yamekamilika na mmiliki ameanza
kuyatumia kwa matumizi ya kiofisi.
Alisema
ujenzi huu umeenda sambamba na uwasilishwaji wa mitambo ambapo mitambo
yote kwaajili ya kiwanda hivi vilivyokamilika vishawasili katika eneo la
kiwanda huku zikisubiria wataalamu kutoka Italia kuja kuzifunga.
Awamu ya pili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakta ngozi ukiendelea katika eneo lililopo jirani na Gereza la Karanga mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdalah Ulega akitizama mashine za kuchakata ngozi alipotembelea kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bidhaa za Ngozi ya Kilimanjaro Mhandisi Masud Omari akiumuonesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi moja ya mashine zitakazotumika katika kuchakata ngozi katika kiwanda hicho .
Mashine kwa ajili ya kuchakata Ngozi ambazo zinatarajiwa kufungwa katika kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro .
Na Dixon Busagaga ,Kilimanjaro
Kiwanda kipya kimejengwa katika eneo la hekari 25 lililotengwa katika Gereza la Karanga Manispaa ya Moshi Mjini huku uzalishaji wa kiwanda hiki ukitazamiwa kuzalisha jozi 4,000 za viatu kwa siku sawa na jozi 1,200,000 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment