Wananchi wa Mkoa Simiyu wamesema kuwa wameridhishwa na elimu inayotolewa na Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA katika maonyesho ya Kilimo nane nane yanayoendelea katika viwaja vya Nyakabindi mkoani humo.
Hayo yamebainika mara baada ya wanachi hao kufika katika Banda la TAWA na kupatiwa elimu masuala mbalimbali hasa ya ufugaji wa wanyamapori kufuatia agizo la Mhe Rais Dakta John Pombe Magufuli kuwataka wananchi kufuga wanyamapori.
Akitoa maelezo kwa wananchi hao Mkuu wa kitengo cha habari wa TAWA Twaha Twaibu amewaeleza wananchi hao utaratibu wa kuanzisha mashamba,bustani na ranchi za wanayamapori kwa mujibu wa sharia.
Twaha amesema kuwa mambo ya msingi wa kuzingatia wakati wa kuhitaji kufungua maeneo ya ufugaji wa wanyamapori ni pamoja na kuwa na eneo la mradi,kuwa na andiko la mradi,kupata ushauri wa wataalamu kuhusu mradi uliopendekezwa .
Mengine ni pamoja kusajili mradi kwa BRELA jina la biashara au kampuni pamoja na kuhakiki eneo ikiwa ni pamoja na kufanya tathimi ya athari ya mazingira ya mradi pendekezwa.
Sanjari na hayo amesema kuwa baada ya kupewa leseni,mradi wa ufugaji wa wanayamapori unatakiwa kusajiliwa uhai wa usajili wa miaka 15
Aidha TAWA katika maonyesho hayo imetoa elimu kuhusu uanzishwa wa mabucha ya kuuza nyamapori.
Hata hivyo Mkuu wa kitengo cha habari wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Twaha Twaibu amewataka wananchi kuwa na utarabu wa kutembea vivutio hasa vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment