Matokeo chanyA+ online




Thursday, September 17, 2020

KITUO CHA AFYA MKAMBA KUPATIWA GARI YA KUBEBEA WAGONJWA



Na. Scolastica Msewa, Mkuranga.
Wananchi wa tarafa ya mkamba wilayani mkuranga mkoani pwani wameahidiwa kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya mkamba kilicho boreshwa ikiwa ni pamoja na kujaziwa vifaa, na kuletewa daktari wa upasuaji ili kuendelea kutoa huduma bora.

Ahadi hiyo imetolewa na mgombea ubunge wa Jimbo la mkuranga na naibu waziri wa mifugo Na uvuvi abdalah Ulega wakati alipofanya kampeni katika Kata ya mkamba, bupu na panzuo zilizopo katika tarafa hiyo na kusema kituo cha afya mkamba kilikuwa na halimbaya wakati anaingia madarakani lakini kwa juhudi za daktari John pombe magufuli Sasa kimeboreshwa.

Ulega amesema ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 21/25 kila kituo cha afya nchini kitapatiwa gari kwa ajili ya kubebea wagonjwa.

Aidha Ulega amesema kipaumbele chake kwa miaka mitano ijayo ni kuhakikisha barabara mkamba zinafunguka ili kukuza uchumi wa wananchi hao, ambapo awali barabara ya kimanzichana mkamba ilipata milioni 400 na kufanikiwa kuziba madimbwi na mabonde yaliyokuwepo ikiwemo kiyembayemba na  inapitika muda wote.

Hata hivyo ulega amesema anaenda kuinua kiwango cha elimu mkamba kwa kujenga mashule ambapo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa shule ya nyekenge, lengo nikuhakikisha mkamba inapata wasomi wengi.

Amesema moja ya mikakati yake ni kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkamba na kuwapatia vijana wamkamba mashine za ufundi seremala ili wakashindane kiuchumi.

Kwa upande wa kinamama ulega amesema ameahidi kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba ili waendeleze shughuli zao za ujasiria mali.


No comments:

Post a Comment