Matokeo chanyA+ online




Wednesday, September 16, 2020

SERIKALI IMETEKELEZA MIRADI YA MAJI 154 KATIKA MKOA WA KAGERA


 

Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe amesema serikali imetekeleza miradi ya maji 154 katika mkoa mzima wa Kagera ili kumaliza tatizo la uhaba wa maji.

Amesema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika
viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera na kuongeza kuwa kuna mradi wa maji vijijini kupitia Buwasa yenye thamani ya shilingi bilioni 50.71 na miradi mingine inatarajiwa kukamilila Novemba 2020 ili kusambaza maji katika maeneo yote.

"tunataka upatikanaji wa maji uongezeke ufike mpaka asilimia 87.6 kwa upande wa mijini na mpaka sasa hivi iko miradi 18 inayosimamiwa na Buwasa ambayo inagharama ya shilingi bilioni 59.04 ukiwemo mradi wa Bukoba manispaa unaogharimu shilingi bilioni 32 na miradi mingine inaendelea kutekelezwa ukiwemo ule Kyaka-Bunazi utakao gharimu bilioni 15 .1" amesema Rais Magufuli



 


Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Kagera katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 16 Septemba, 2020

 




Sehemu ya Wananchi wa mkoa wa Kagera waliokusanyika katika Viwanja vya Gymkhana kumsikiliza Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Septemba, 2020






Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wananchi wa mkoa wa Kagera mara baada ya kuwasili katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 16 Septemba, 2020

 

No comments:

Post a Comment