Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John Magufuli ametuma salam za rambirambi kwa uongozi wa Shule ya Byamungu Islamic wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, kufuatia vifo vya watoto 10 waliopoteza maisha kwa ajali ya moto.
Dkt. Magufuli ametuma salamu hizo wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye
uwanja wa Mazaina wilaya ya Chato mkoani Geita.
"Nimesikitika
sana na taarifa za watoto 10 kufariki kwa moto shuleni Byamungu,
naombeni wote tusimame tuziombee roho za marehemu zipumzike kwa amani,"
amesema Dkt. Magufuli
Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umetokea usiku wa kuamkia leo katika bweni la wavulana katika shule hiyo.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Chato katika mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa utalii umeongezeka nchini "watalii wameongezeka na makusanyo yameongezeka kwa mwaka yamepanda kutoka bilioni 1 mpaka bilioni 2.6 usa dola ni kwasababu tuna ndege zetu, mtu anasimama ameshiba ugali anasema ndege hazina faida yeye alikotoka huko alikuja na bajaji''
Aidha amesema kuwa watanzania wanafahamu walikotoka wanafahamu mahali walipo wanafahamu wanakoelekea.
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Chato katika mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Sehemu ya Wananchi waliofurika katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvisha kofia ya CCM msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize baada ya kutumbuiza kwenye mkutano
wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Mazaina leo Jumatatu Septemba 14, 2020
No comments:
Post a Comment