Vijiji 77 kati ya vijiji 73 vya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera vimepelekewa huduma ya umeme na vijiji 4 bado havina umeme.
Hayo
yamesemwa jana (Jumanne, Septemba 29, 2020) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa
wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Kassambya, katika mikutano
uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.
Amevitaja
vijiji ambavyo havina umeme na vipo kwenye mpango wa kupelekewa umeme
kuwa ni vijiji vya Buchurago, Katano, Kakunyu na Bugango.
Akizungmzia
sekta ya mifugo ambayo imetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020
hadi 2025 kuanzia ukurasa 47-52, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi imeisimamia vizuri sekta ya mifugo ili
kuhakikisha wafugaji wanapata manufaa.
“Shilingi milioni 23
zimetumika kukarabati machinjio ya Bunazi hapa Misenyi, pia
tumerahisisha uuzaji wa mazao ya mifugo kwa kufuta tozo kero 114 katika
sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na kuimarisha masoko ya mazao ya mifugo
kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo,”
alisema.
Alisema Serikali imepanga kuanzisha vituo vya kisasa
vya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika mikoa 18 ambayo haina vituo,
kuimarisha huduma za tiba za mifugo kwa kuhakikisha kila wilaya ina
maabara, kliniki na daktari wa mifugo.
Mheshimiwa Majaliwa
ambaye yuko mkoani Kagera kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya
CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge
wa jimbo la Nkenge, Dkt. Florent Kyombo na wagombea udiwani 13 wa CCM
wa kata za wilaya hiyo. Mgombea udiwani wa kata ya Kassambya, Bw. Yusuph
Jumbe na wenzake sita, wamepita bila kupingwa.
Kuhusu barabara,
Mheshimiwa Majaliwa alisema sh. bilioni 3.57 zilitolewa kupitia Wakala
wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa ajili ya ujenzi na
matengenezo ya barabara za wilaya hiyo zikiwemo barabara za
Bukwali-Kashenye-Bushango, Ngorogoro-Kyabugombe, Mabuye –Itara na
Ruzinga - Mugongo.
Alizitaja barabara nyingine kuwa ni za Gera –
Ishozi – Ishunju, Nyankele – Kilimilire, Mabale–Mwemage-Kyaka,
Nyankele-Nyamilembe–Kenyana na Kituntu–Bwengabo. Alisema mwaka
2020/2021, sh. milioni 711.6 zimetolewa kupitia TARURA kwa ajili ya
ujenzi na matengenezo ya barabara kwa muda maalum.
No comments:
Post a Comment