Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua kahawa ya wakulima katika kiwanda cha Kamahungu kinachomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU) wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Japhet Hasunga tarehe 3 Septemba 2020 amewasili Wilayani
Karagwe katika mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja,
ambapo amekagua shughuli mbalimbali za kilimo.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Karagwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera tarehe 3 Septemba 2020.
Waziri
Hasunga amekiagiza Chama Kikuu cha Ushirika Karagwe (KDCU) kuwalipa
wakulima malipo yao ambapo ametoa siku tatu kuanzia tarehe 4 Septemba
2020 mpaka Septemba 6, 2020 Jumla ya Bilioni 7.8 ziwe zimelipwa haraka.
Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Mjini Karagwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020.
Ametoa maagizo hayo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wataalamu wa Wilaya ya
Karagwe huku akikitaka Shirika la ukaguzi wa hesabu za vyama vya
Ushirika (COASCO) kukamilisha ukaguzi wa vyama vya Ushirika ndani ya
wiki mbili ili wakulima waweze kulipwa fedha zao za malipo ya nyongeza,
Kadhalika ameitaka COASCO kupitia hesabu zao ili waweze kutoa taarifa.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera Leo tarehe 3 Septemba 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kagera
Hasunga amesema kuwa ni Marufuku kuchelewesha malipo ya wakulima badala yake Bodi ya Kahawa kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania inapaswa kubainisha njia bora ili kurahisisha malipo ya wakulima.
Vilevile, Waziri Hasunga ameitaka Bodi ya kahawa kujenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha unywaji wa kahawa wa ndani kwani kufanya hivyo kutaongeza soko la ndani la kahawa.
No comments:
Post a Comment