Matokeo chanyA+ online




Friday, October 2, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU BRITON WILFRED MOLLEL ALIYEUWAWA TUNDUMA MKOANI SONGWE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kuwapa pole Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel (26) Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM aliyeuwawa tarehe 25 Agosti 2020 Tunduma mkoani Songwe, kulia ni Mama Mzazi wa Marehemu Roda Bryson Mwaisongole akiwa pamoja na mke wa Marehemu Salome Philemon Mayao.  Tunduma mkoani Songwe leo tarehe 02 Oktoba 2020.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi rambirambi yake ya Sh. Milioni 3 Mama Mzazi wa Marehemu Briton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe ili ziwasaidie katika kipindi hiki kigumu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi rambirambi yake ya Sh. Milioni 3 mke wa Marehemu Briton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama Mzazi wa Marehemu Briton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe. 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel, kulia ni Mama Mzazi wa Marehemu Roda Bryson Mwaisongole, mke wa Marehemu Salome Philemon Mayao pamoja na Watoto wake wawili. Marehemu Briton aliuwawa tarehe 25 Agosti, 2020 Tunduma mkoani Songwe na ameacha Watoto watatu. Marehemu Briton alikuwa Mkuu wa Mafunzo na Mkuu wa Itifaki UVCCM Wilaya Momba

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mkono Watoto wawili wa aliyekuwa Mwanachama wa CCM Marehemu Briton Wilfred Mollel Tunduma mkoani Songwe leo tarehe 02 Oktoba 2020.  PICHA NA IKULU

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Oktoba, 2020 amekutana na familia ya kijana Briton Wilfred Mollel (26) aliyeuawa kikatili tarehe 25 Agosti, 2020 baada ya kushambuliwa katika vurugu zilizotokea wakati wa urejeshaji wa fomu za kugombea udiwani kwa msimamizi wa uchaguzi wa Kata ya Kaloleni katika Jimbo la Tunduma Mkoani Songwe.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mama wa Marehemu aitwaye Roda Bryson Mwaisongole na Mjane wa Marehemu aitwaye Salome Philemon Mayao Mjini Tunduma ambapo amewapa pole na kutoa ubani wa shilingi Milioni 6.

Marehemu Briton Wilfred Mollel aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alimsindikiza mgombea udiwani wa CCM katika kata ya Kaloleni wakati wa urejeshaji wa fomu siku ya tukio.

Mhe. Rais Magufuli amelaani mauaji hayo na ameagiza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote waliohusika. 

Mhe. Rais Magufuli na wanafamilia hao wamefanya sala fupi ya kumuombea Marehemu apumzike kwa amani, Amina.

Marehemu Briton Wilfred Mollel ameacha Mke na watoto 3 wenye umri wa kati ya mwaka 1 na miaka 6. 

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli ambaye amewasili Mjini Unguja (Zanzibar) amemtembelea na kumjulia hali Bw. Hamis Nyange Makame (63) aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja akitibiwa majeraha baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni wakati akiswali Msikitini huko Kangagani, Wilaya ya Wete (Pemba).

Bw. Hamis Nyange Makame (Prof. Gogo) ambaye ni mwanachama wa CCM alishambuliwa tarehe 22 Septemba, 2020.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na shambulio hilo la kikatili na ameviagiza vyombo vya dola kuchukua hatua zinazostahili kwa wote waliohusika.



 

No comments:

Post a Comment