Matokeo chanyA+ online




Thursday, October 1, 2020

SERIKALI YABORESHA MAKAZI YA WAZEE NCHINI



Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Tunduma katika mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika katika viwanja wa Nyerere Tunduma mkoani Songwe leo tarehe 1 Oktoba 2020.


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa wazee wanaotibiwa bure nchi nzima ni 1,042,403 amesema hayo katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Nyerere mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe.

Amesema kuwa kwasasa Serikali imedhibiti mauaji ya wazee katika maeneo mbalimbali hasa kanda ya ziwa kwa kuviagiza vyombo ulinzi na usalama kudumisha amani na utulivu wa wazee pamoja na watanzania wote.

Aidha, amesema kuwa serikali imeboresha makazi ya wazee kwa kukarabati na kujenga miundombinu katika maeneo kolandoto mkoani Shinyanga, Nunge Dar es salaam, Njoro Kilimanajaro, Magugu Manyara na Funga funga mkoani Mara.


Makazi ya Wazee yaliyoboreshwa ya Kolandoto, nyumba hiyo yenye vyumba 14, sebule, bustani, miundombinu ya maji na umeme imejengwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Idara ya Maendeleo ya jamii na kusimamiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi kwa gharama ya sh. milioni 138.1, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa jiko la kisasa linalotumia nishati ya gesi.


Wananchi wa mji wa Tunduma mkoani Songwe wakimsikiliza Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli



No comments:

Post a Comment