Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameongoza Kikao Maalum cha
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao hicho kimefanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar iliyopo Kisiwandui.
Pamoja na mambo
mengine kikao hicho kimejadili mapendekezo ya WanaCCM wanaoomba
kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Katiba
ya Zanzibar ya mwaka 1984,ibara ya 73 Spika wa Baraza la wawakilishi
anaweza kuchaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
au mtu mwenye sifa za kuchaguliwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein na (kulia kwake ) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Mhe Balozi Seif Ali Iddi na (kushoto ) Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi wakiwa wamesimama walipowasili katika
ukumbi wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,
kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Jijini Zanzibar jana 2/11/2020.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi
Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini
Pamoja na hayo kwa
mujibu wa kanuni ya 5 ya kanuni za Baraza la Wawakilishi toleo la mwaka
2020 zinaeleza kwamba kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu
kinaweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika kwa kuwasilisha jina la
mgombea wake Time ya Uchaguzi,hivyo basi CCM inawajibika kufanya
mchakato wa ndani ili kupata jiba la mwanachama mmoja atakayegombea
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Katika Kikao hicho
kimepokea na kujadili majina ya Wanachama waliojitokeza kuoomba
kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi mwaka 2020.
Aidha,Kikao hicho
kitatoa mapendekezo yake juu ya wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea
nafasi ya Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar kwa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa kuteua jina la mwanachama mmoja atakayegombea nafasi ya Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Akizungumza Dk.Shein,
alisema matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 yamevunja rekodi toka
enzi za ASP hadi hivi sasa wakati wa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Alisema wagombea wote wa CCM walikuwa imara na wana sera zinazouzika kwa wananchi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohameed
Shein akifungua Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM
Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCK Kisiwandui
Jijini Zanzibar 2/11/2020.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Zanzibar na Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe Dk. Ali Mohameed
Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla
Juma Mabodi alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Jijinin Zanzibar kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmaashauri Kuu
ya CCM Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Jijini Zanzibar , kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi
Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar 2/11/2020.
Wajumbe Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakipitia makamrasha yao kabla ya kuaza
kwa Kikao hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na
Rais Mstaaf wa Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kilichofanyika
katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Picha na Ikulu
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
Pamoja na hayo
aliwasihi wajumbe hao kutobweteka na ushindi uliopatikana badala yake
waanze mapema kujiandaa na uchaguzi ujao baada ya miaka mitano.
Aliwashukru Wana CCM
wote na wananchi kwa ujumla waliofanya maamuzi sahihi ya kuichagua CCM
ili iwaletee maendeleo endelevu kisiasa,kiuchumi na kijamii.
Alieleza kuwa amefika
ukomo wa utumishi wake wa kiti cha Urais kwa mujibu wa matakwa ya
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,na kumkabidhi mrithi wake ambaye ni
Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi nchi ikiwa katika mikono salama
ya CCM hivyo anatakiwa kuendelea kulinda tunu za Muungano na Mapinduzi
ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Akizungumza Makamu
mstaafu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliwashukru na
kuwaaga wajumbe wa Kamati Maalum na kuwasihi waendelee kushirikiana na
kushikamana ili CCM iendelee kuwa imara zaidi.
Naye Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi, alisema CCM ina deni kwa
wananchi la kutekeleza ahadi zake pamoja na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2020/2025.
Kikao hicho kimeudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.
No comments:
Post a Comment