Mbunge Jimbo Chalinze, Ridhiwani Kikwete akishiriki zoezi la kuchimba msingi unaotarajiwa kujengwa jengo la madarasa mawili yatakayosaidia kupokea wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo katika shule ya sekondari ya Kiwangwa.
Mbunge Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema muda wa kazi ni sasa, hakuna kulala
wala likizo ilikuwatumikia watanzania wanyonge.
Ridhiwani ambaye amekuwa katika shughuli mbalimbali za Kijimbo, ambapo tarehe 27 Desemba 2020 licha ya kuwa ni siku ya mapumziko, ameweza kufanya ziara ikiwemo kukagua shule za Sekondari zaidi ya 6 pamoja na ukaguzi wa soko la kisasa linalojengwa Bwilingu-Chalinze Mjini.
Mbunge Jimbo Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa pamoja na watendaji wengine wakiangalia msingi unaotarajiwa kujengwa jengo la madarasa mawili yatakayosaidia kupokea wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo katika shule ya sekondari ya Chalinze.
Awali
akikagua soko hilo na kujionea maendeleo yake pia aliweza kuonana na
baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo Jumuiya ya wachinjaji kuku na nyama.
"Mkandarasi
ametuhakikishia ujenzi unaendelea vizuri na kwa kasi. Pia nimepata
kukagua vizimba vyake katika soko hili ambalo litakuwa kitega uchumi
ndani ya Halmashauri yetu.
Mbunge Jimbo Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa pamoja na watendaji kutoka Halmashauri ya Chalinze wakikagua bweni la kisasa la wanafunzi wa kiume shule ya sekondari Msata.
Mbali na ukaguzi
wa soko hilo, pia Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya kukagua
utekelezaji wa Ilani na Maagizo ya viongozi kuhusu mustakabali wa
Tanzania ya agenda ya Elimu huku akiambatana na Watendaji wa Idara ya
Elimu Sekondari na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani
Possi.
"Tumetembelea shule 6 ikiwemo shule ya sekondari Chalinze, Chahua,Msata, Kiwangwa, Changalikwa, Rupungwi na Mandela wasichana.
"Tumeshuhudia maendeleo makubwa yaliyokwisha fanyika ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni na ofisi za walimu" Alisema Ridhiwani Kikwete na kuongeza:
Pamoja na hayo Mbunge ameshuhudia ujenzi wa madarasa 17 unaoendelea katika maeneo mbalimbali yanayotaraji kukamilika kabla ya tarehe 17 ili yawe tayari kutumiwa katika mwaka mpya wa Elimu.
Ziara ya Mbunge inaendelea katika Kata mbalimbali.
Good job MH.pongezi sana
ReplyDelete