Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein
Ali Mwinyi amewataka Wana CCM na wananchi kwa ujumla kumvumilia wakati
akifanya maamuzi magumu dhidi ya watu wanaoshiriki kufanya vitendo vya
rushwa,uhujumu uchumi na ufisadi wa mali za umma.
Alisema hatovumilia watendaji wanaoshiriki vitendo vya rushwa vinavyosababishia hasara serikali.
Amesema,
yapo mambo yasipofanywa kwa maamuzi magumu basi huko mbele kutakuwa
kugumu na yale maendeleo ambayo yamekusudiwa kufanyika hayatofikiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na
Wanachama wa CCM wa Mkoa wa Kusini Pemba kichama katika ziara yake ya
kutoa shukrani kufuatia ushindi wa CCM wa uchaguzi mkuu uliofanyika
octoba 28,mwaka huu.
DK,
Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa
ya CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchama wa Chama
cha Mapinduzi kisiwani Pemba, mkutano wa shukrani kwa wana CCM baada ya
uchaguzi mkuu, katika ukumbi wa shule ya Fidel Castro mkoa wa Kusini
Pemba.
Alisema katika maendeleo ya watu hatokuwa na muhali kwani
Zanzibar kumezoeleka tabia hiyo ambapo kila anayeguswa utaambiwa ni
mtoto wa fulani ama ana undugu na watu fulani huku nchini ikiendelea
kufilisiwa kwa vitendo vya uhujumu wa mali za umma.
Alisema amekaa madarakani kwa mwezi mmoja na nusu lakini kila anapogusa kumejaa vitendo vya ufisadi.
''Nitafanya
maamuzi magumu lakini sotofukua makaburi wala kutafuta mchawi , lakini
baada ya maamuzi hayo kila senti ya fedha za umma itaheshimiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na Wanachama wa CCM wa Mkoa wa Kusini
Pemba kichama kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Rais wa
Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi katika ziara yake ya kutoa shukrani kwa
wanachama hao iliyofanyika ukumbi wa Fidel Castro Pemba.
DK.
Mwinyi pia alisema, sasa wanazungumzia miradi ya maendeleo ambayo ni
miradi ya fedha nyingi ikiwa ni pamoja na miradi ya ZUSP wenye dola
milion 93, mradi wa maji karibu dola milion 90, na mirandi mingine
itakayokuja ya muendelezo wa ZUSP wenye dola milion 110.
Hivyo
alisema, asipochukua maamuzi magumu sasa, basi fedha hizo zitafujwa na
kuahidi kusimamia miradi hiyo ili waweze kupata thamani katika fedha
zitakazotumika.
Aidha alieleza kuwa, wakati wa kampeni alisema
kwamba amegombea nafasi hiyo kwa dhamira moja ya kuwatumikia wananchi na
kwamba sasa ameshapata uongozi hivyo anayodhima kubwa kwa Mwenyezimungu
na kwa wananchi ya kutekeleza aliyoyaahidi.
"Sasa leo tukiwa tunatekeleza tuliyoyaahidi alafu kuna mtu anatubomoa, kumuacha itakuwa tumejitakia sisi wenyewe," alisema.
Aidha alisema, anayasema hayo kwa madhumuni ya kuwatayarisha wananchi kwa watakaokuja kuyasikia katika kipindi kifupi kijacho, kwani yapo maovu yanayofanywa na yasipowekwa sawa wataendelea kuishi katika uovu.

Baadhi ya Wanachama wa CCM wa Mkoa wa kusini Pemba kichama wakisikiliza
kwa makini hotuba ya shukrani iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika ziara
yake ya shukrani katika Mkoa wa Kusini Pemba kichama huko ukumbi wa
Fidel Castro.
(PICHA NA IS-HAKA OMAR) ATOA SHUKRANI KWA WANA CCM
DK.
Mwinyi pia aliwashukuru wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi
kwa kazi kubwa na nzuri waloifanya katika uchaguzi mkuu uliopita.
"Nimekuja kutoa pongezi kwa sisi sote, tumefanya kazi nzuri, tumefanya kampeni za kisayansi za aina yake, tumefika kwa wananchi wote nyumba kwa nyumba na nakumbuka nilisimama hapa nikatoa jukumu maalum kwa ndugu zetu mabalozi, kwa kweli waliibeba ile kazi na wameenda kuifanya nawashukuru sana," alisema.
Aidha alitoa pongezi kwa wanachama na wananchi kwa ushindi wa kishindo uliopatikana, ambao umeandika historia na kuahidi kuwa ataivunja historia hiyo.
Alisema, kwa kazi ambayo itafanywa na serikali ya awamu ya nane ndani ya miaka mitano basi wataivunja rekodi ya uchaguzi wa mwaka 2020 ifikapo uchaguzi wa 2020.

"Hii
ni rekodi imewekwa mpaka sasa hivi, lakini nataka nikwambieni rekodi
hii itavunjwa kwa utendaji ambao tutaingia nao katika kipindi hiki cha
miaka mitano," alisema.
DK. Mwinyi alisema, kipindi cha kampeni walihubiri sana swala la amani na kwamba amani ndiyo msingi wa maendeleo wa nchi yeyote ile, na kuwapongeza viongozi wa dini wa madhehebu yote waliyoiombea amani.
Mbali na hayo Rais Mwinyi alisema, baada ya uchaguzi walifanya kazi ya kuwaunganisha watu kwa makusudi kwa lengo la kuleta umoja ndani ya nchi, na ndio maana wakakubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
"Sasa najua bado hili gumu, kwani wapo watu wa pande zote mbili, upande wetu wa CCM na upande wa wenzetu ambao bado hawalipendi hili jambo, lakini mimi nakwambieni tukitaka kuleta maendeleo tunayoyazungumzia lazima tuunganishe watu," alisema.

alisema, amekuja kuwasihi wanachama wa CCM, kukubaliana na maamuzi hayo
waliochukua ya kuunganisha wananchi wote Unguja na Pemba ili waweze
kuwa kitu kimoja na kuondokana na malumbano ya kisiasa na badala yake
ibaki kazi moja tu ya kuleta maendeleo.
Alisema, hata kwenye vitabu vya dini vimesema, 'Tumeambiwa tuunde udugu, tuwe wa moja na tusilete mafarakano na umoja ndiyo dini', hivyo alisema maamuzi ya kuungana ni kwa lengo la kuwa wamoja.
Aidha alisema, yeye hana shaka yeyote kwamba kwa amani hii iliyokuwepo na makubaliano ya kuleta umoja waliyoyafanya basi kazi ya kuleta maendeleo itakuwa nyepesi.
Rais Mwinyi aliahidi kuwa kazi ya kuleta maendeleo itafanyika, kwani baada ya uchaguzi na baada ya kuwaunganisha watu pamoja basi kazi iliyo mbele ni kuleta maendeleo kwa wananchi.

Alisema, maendeleo yataletwa
katika mambo mawili, moja ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha
Mapinduzi na pili ni ahadi walizozitoa wakati wa kampeni.
"Na mimi nataka niseme kwamba tumetoa ahadi nyingi na tumeziandika hatujazisahau hata moja, leo nasimama mbele yenu nasema kwamba nimedhamiria kutekeleza ahadi zote tulizo ahidi wananchi," alisema.
Alisema, ameanza kuunda serikali, lengo lake likiwa ni kuhakikisha kwamba wale wote anaowateua wanamsaidia katika kuhakikisha kwamba wanantekeleza ahadi zao walizozitoa.
Akizungumzia ahadi alizotoa ndani ya Chama chake wakati wa Kampen DK. Mwinyi alisema, ahadi zote zipo pale pale na kwamba atatekeleza na wachama watazisikia salamu zake hivi karibuni.
"Ndugu zangu wana CCM leo nimekuja kutoa shukrani, nakushukuruni sana kwa kazi nzuri sana tuloifanya na kufanikiwa kushinda na kuvunja rekodi ya ushindi katika nchi yetu," alisema.

Alisema, amekuja kutoa
shukrani, pongezi na kuomba msaa da kwao kwamba sasa wanaanza kazi ya
kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na ahadi zao na kwamba bado
viongozi wa CCM wana wajibu wa kuwasaidia.
"Nyinyi ndiyo macho yetu kule mlipo na ahadi zetu tunapotaka kuzitekeleza ikiwa ipo kule kijijini au kule wilayani basi mambo yakiwa ovyo nyinyi muwe kwa kwanza wa kusema," alisema.
Aidha alisema yake yote aliyoyasema atafanya basi bila ya shaka atayafanya na kukumbusha ahadi yake aliyosema kuwa atakifaya kisiw cha Pemba kuwa ni eneo maalum la uwekezaji.
Alisema, nia yake ni kwamba maendeleo yanayopatikana Unguja yaende sambamba na maendeleo ambayo yatapatikana Pemba.
Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kusini Pemba alimuahidi kwa niaba ya wana CCM wenzake kuwa, hayo yote aliyaeleza kuwa wapo pamoja na yeye na kuahidi kumfichulia maovu yote.

"Usiwe na wasi wasi kwani mambo mazito utayaona kwani yatakapotoka hayo ndiyo mafanikio makubwa ya nchi yetu," alisema.
No comments:
Post a Comment