Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA)
Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Mahafali ya 16
ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Dk. Ali
Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja 30-12-2020.(Picha na
Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametawazwa kuwa Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Ndg. Mwita Mgeni Mwita na (kulia
kwa Rais) Makamu Mkuu wa Chuo Dkt.Zakia Mohamed Abubakar, hafla hiyo
imefanyika wakati wa Mahafali ya 16 ya SUZA yaliofanyika katika ukumbi
wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja 30/12/2020.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa Katika Sayansi za Tiba Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliofanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu 30-12-2020.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment