Mbunge amesema hayo wakati wa ziara maalum ya Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango inayotembelea miradi mbalimbali ya Halmashauri ya Chalinze mapema.
Ridhiwani Kikwete amewahakikishia Wafanyabiashara hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Shabani Mazengo kuwa ni shabaha yake kuona wanyonge waliojitolea kupisha ujenzi huo wanaenziwa kwa kupewa nafasi ya kipekee kwenye soko hilo.
Mhandisi wa Halmashauri ya Chalinze, John Chiza (katikati) akimuonesha mchoro wa soko la kisasa la Bwilingu, Mbunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kushoto), wengine ni Wajumbe Kamati ya Uchumi, fedha na mipango.
Akiongea na wafanyabiashara hao akiwa na viongozi wenzake Mhe. Ridhiwani Kikwete alisema:
"Wafanyabiashara waliokuwa hapa awali kuamua wenyewe kuvunja vibanda vyao kwa hiyari ambao wanapata 180, ndio wawe wa mwanzo kupewa nafasi hapa kisha wengine ndio wafuatie" Alisema Ridhiwani Kikwete.
Muonekano wa baadhi ya eneo la soko hilo linalojengwa
Mbunge aliongeza kuwa:
"Kwa sasa soko lipo katika hatua nzuri hadi mwezi wa Nne mwaka huu
linatarajiwa kukamilika na litakuwa la kisasa zaidi" alisema Ridhiwani
Kikwete.
Ridhiwani Kikwete alieleza kuwa ujio wa soko hilo ni
baada ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutoa maagizo kuwa miji
yote mikubwa iwe na masoko, Hospitali kwa maana (Vituo vya afya), hivyo
wao kama halmashauri ya Chalinze wanaendelea na utekelezaji wa ilani
kwa soko hilo.
Mbunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Geofrey Kamugisha (mwenye koti jeusi) wakati wa kukagua mipaka inapojengwa soko jipya la kisaa la Bwilingu
"Maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt.
Magufuli ambapo pamoja na yote yana nia njema ya kuongeza mapato ndani
ya Halmashauri yetu ya Chalinze na ustawi wa Wananchi wetu ambao
watapata fursa ya huduma bora ndani ya soko hili" Alisema Ridhiwani
Kikwete.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,
Geoffrey Kamugisha alisema wametembelea kujionea miradi ya maendeleo
ikiwemo ujenzi wa soko hilo la kisasa na choo.
Na. Andrew Chale, Chalinze
"Kamati
tumetembelea na ujenzi huu ambao kwa Soko unagharimu kiasi cha Tsh.
Milioni 449. Tunapongeza hatua kubwa iliyofikiwa hivyo tunaomba
mkandarasi kuhakikisha ubora wa kazi na mapendekezo yaliyotolewa katika
ujenzi yanazingatiwa." Alisema Kamugisha.
Ziara hiyo pia iliendelea kwa kamati hiyo ya Uchumi, Fedha na Mipango pia ilitembelea uzio wa Kituo cha Afya Chalinze na kumalizia ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chalinze la Wakulima na Wafugaji katika viwanja vya Nane Nane, Morogoro.
No comments:
Post a Comment