Wafugaji
nyuki na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki nchini wametakiwa kuimarisha
na kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika ili waweze kunufaika na
huduma zitolewazo na vyama hivyo.
Wito huo
umetolewa jana Januari 5,2021 na Kamishna Msaidizi - Ufugaji Nyuki,
Hussein Msuya alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa Jukwaa la Ufugaji
Nyuki nchini – TABEDO katika ukumbi wa Chuo cha Ushirika Moshi tawi la
Dodoma.
Msuya alisema, baada ya Serikali kufuta
kampuni zenya ukomo wa ahadi na yasiyo na mtaji ambayo hayafanyi
shughuli za kukuza biashara na ukwekezaji yaliyokiwa yamesajiliwa na
msajili wa Makampuni (BRELA). TABEDO ikiwemo, imelazimika kukutana na
wanachama wake kwa lengo la kujadili hatma yao na kuunda kamati
itakayokwenda kufanya tathimini ya vyama vya msingi vya ushirika wa
wafugaji nyuki nchini.
“Hivi sasa hatuelewi
“status” ya vyama vya msingi hivyo kamati hii itakayokwenda kuundwa leo
itafanya tathimini kuona ni nini kinaendelea, tukishaelewa sasa tutaenda
kuangalia ni nini hasa kilichopelekea vyama hivi kusinzia au kufa,
“na
kwa kushirikiana na watu wa ushirika kamati itaangalia ni mambo gani
itafanya kuhakikisha vyama hivi vinasimama na kushauri namna bora ya
kuunda muunganiko utakakuwa mbadala wa TABEDO na kuja na mfumo mwingine
wa kuunganisha vyama vya mushirika vya msingi” anasema Kamishna
Msaidizi huyo.
Msuya alitoa wito kwa wananchama
kutoa ushirikiano kwa kamati itakayoundwa ili kujitendea haki kwa kile
alichokisema “unakata mti unapanda mti sio unaenda kulala”.
Azima
ya kukuza viwanda haitatimia ikiwa hakutakuwa na ushirika wa wafugaji
nyuki ulio imara, ushirika wa wafugaji nyuki utawezesha kuapta nguvu ya
kukuza mitaji na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki, ambayo ni
malighafi ya viwanda vya mazao ya nyuki.
Rudia
Issa ni Mwenyekiti wa iliyokuwa TABEDO anasema wako tayari kushirikiana
na kamati itakayoundwa ili kuweza kuunda vyama vya ushirika
vitakavyokwenda kutoa ufumbuzi wa mahitaji ya wafugaji nyuki nchini.
Alisema
kila mfugaji nyuki akitambua umuhimu wa kuwa mwanachama wa ushirika,
atanufaika na mafao mbalimbali ikiwamo kupatiwa mikopo kutoka katika
taasisi za fedha pamoja na soko la uhakika la mazao yake.
Lemiona
Kimeshua ni mfugaji nyuki na mwananchama wa TABEDO anasema aliacha
shughuli za ufugaji nyuki na kubaki kuwa mnunuzi kutokana na kulegalega
kwa vyama vya ushirika lakini kutokana na mkazo mkubwa wa Serikali
kwenye sekta hiyo ameamua kufufua na kuanzisha mashamba mapya ya nyuki.
Rudia
Issa ni Mwenyekiti wa iliyokuwa TABEDO akiwasisitizia wanachama wake
umuhimu wa kujiunga na Chama vya ushirika vilivyopo na vile
vitakavyoanzishwa.
Kamishna
Msaidizi - Ufugaji Nyuki, Hussein Msuya akiwaeleza Mipambo mbalimbali
ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika kuhakikisha wananufaika na
fursa mbalimbali wanazozitoa kwa vikundi na kuwataka wajiunge ili
waweze kuwa na sifa wakunufaika.
Wajumbe wa mkutano
Wajumbe wa mkutano
Mjumbe wa mkutano
Wajumbe wa mkutano
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TBEDO Ayubu Kamwaga na Mwenyekiti wake Rudia
Issa ni wakicheka kwa Furaha baada ya kuthibitishiwa kuzaliwa uya kwa
chama hicho kama chama cha ushirika baada ya kufutwa rasmi na Serikali
kwa mujibu wa Sheria.
No comments:
Post a Comment