Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa akifungua kongamano kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.
Mtafiti Mkuu wa mradi wa GRILI Dkt. Faith MabikiAkileza malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo la wadau wa tiba asili nchini.
Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi na Elimu Dkt. Geofrey akitoa salamu za Ndaki yake na kuwakaribisha wageni hao Chuoni hapo.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa (Katikati) akisikiliza maelezo toka kwa viongozi wa mradi, Prof. Samweli Kabote amabye ni Muwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na fedha (Wa kwanza Kushoto) Akifuatilia hotuba ya ufunguzi, W KWANZA Kushoto ni Dkt. Geofrey Kalugila Rasi wa ndaki ya Solomon Mahlangu ya sayansi na Elimu.
Na Calvin
Gwabara, Morogoro.
WAGANGA wa Tiba Asili nchini wametakiwa kuangalia kwa undani namna ya kutumia matokeo ya
tafiti zinazofanywa na watafiti wa Chou Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi
zingine ili kuboresha bidhaa zilizopo na kuanzisha bidhaa mpya ili kuendana na
mahitaji ya jamii kwa wakati sahihi.
Wito huo ulitolewa
na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Utawala na
Fedha Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba
ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akifungua Kongamano
la siku moja la Watalaamu wa Tiba asili na kutoka maeneo mbalimbali nchini
lililofanyika Chuoni kabla ya maonesho na uzinduzi wa jukwaa la ubunifu wa
bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa lililoandaliwa na Mradi wa GRILI.
Prof.
Mhairwa alisema kuwa njia hiyo ni muhimu sana hasa katika wakati huu ambao
dunia inahangaika kutafuta chanjo na tiba ya ugonjwa wa COVID 19 ambapo dawa za
mimea zimeonekana kufanya vizuri Zaidi kuliko za hospitalini,
”
Wanasayansi na waganga wa tiba ya asili sio kama vyama viwili vya upinzani,
sisi tunafanya kazi kwa kutegemeana, sisi tunavitu tunavumbua kisayansi lakini
pia kuna vitu vingine tunavifanyia utafiti vile ambavyo mmevianzisha nyinyi ili
kuweza kupata udani Zaidi wa dawa mnazogundua kwahiyo hatupingi kazi zenu wala
msituone kama vile maadui sisi tufanye kazi kwa pamoja kwa faida ya jamii na
taifa letu” Alisisitiza Prof. Mhairwa.
Alisema
bidaa za mimea dawa zinakabiliwa na changamoto zinazohusiana na
uzalishaji,uvunaji,utengenezaji,uuzaji na upatikanaji endelevu wa malighafi hivyo
ili kupunguza changamoto hizo na kuzindoa kabisa kunahitajika utafiti Zaidi wa
kisayansi,ubunifu Zaidi katika masoko,uzingatiaji wa hali ya juu wa vigezo vya
ubora vinavyotakiwa na kufuata taratibu za biashara zenye tija.
Lakini pia aliwataka
Wataalamu hao wa Tiba asili kuangalia masuala ya kisera yanayoleta changamoto
katika kuhaulisha teknolojia hizi ili ziweze kutumika kibiashara na kuanzisha
viwanda vya uzalishaji wa mimea dawa na hasa katika kipindi hiki ambapo sera ya
serikali ni kusukuma uanzishwaji wa viwanda kwenye sekta hii.
Naibu Makamu
huyo wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha aliwahakikishia kuwa SUA na hasa
kurugenzi ya uzamili,Utafiti,Uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu
kwa kushirikiana na serikali wataendelea kuwa nao bega kwa bega kwa kusaidia
jitihada za wadau wote kwenye sekta hii katika kuboresha tafiti za oaina hii
kwa kadri mazingira yatakavyoruhusu.
Akitoa
salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Mratibu wa
Utafiti na machapisho katika kurugenzi ya shahada za
uzamili,utafiti,uhaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu ya Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Japhet Kashaigiri alisema kuwa kurugenzi hiyo
na vitengo vingne vya SUA vimekuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya aina
hiyo ili kujaribu kuboresha biashara za mazao ya Kilimo,Ufugaji na Misitu kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta hizo.
“Katika
makongamano haya SUA imekuwa ikishirikisha wasimamizi na wakaguziwa ubora wa
biashara hizi pamoja na watunga sera kwa ujumla na utaratibu huu umeongeza
mchango mkubwa wa chou chetu katika kutatua changamoto mbalimbali na kuboresha
biashara za mazao nah ii ni muhimu hasa katika awamu hii ya serikali ya tano
ambayo mwelekeo wake ni kuwa uchumi wa viwanda.
Prof.
Kashaigili alisema Vyuo Vikuu kote duniani ni vitovu vya maendeleo ya kitaaluma
na Tafiti mbalimbali na kwa muktadha huo kurugenzi ya uzamili kupitia kitengo
chake cha uhaulishaji wa teknolojia pamoja na mradi wa GRILI zimeona ni vyema
kutumia uzoefu wake wa ndani na kwa kushirikiana na wadau wengine kuandaa
kongamano hili hapa SUA ili kuwaleta wadau wote pamoja na kujadili namna ya
kukuza uelewa na kutatua changamoto hizo.
Akileza
malengo ya mradi huo wa GRILI na malengo ya Kongamano hilo Mtafiti mkuu wa
mradi huo Dkt. Faith Mabiki amesema Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwaka 2018
ukiwa na lengo la kuchangia katika kuongeza ubora wa bidhaa za miti dawa ili
kuboresha Maisha ya watengenezaji,afya za watumiaji na kuchangia katika pato la
taifa.
Dkt. Mabiki
alisema ili kufikia malengo hayo ya muda mrefu mradi huo unajenga uwezo wa
kitafiti wa kitafiti kwa wanafunzi wa shahada za uzamivu 5 na shahada za
uzamili 2 katika maeno muhimu ya kemikali,usugu wa dawa na masoko na unategemea
kutoa matokeo ya kitafiti yatakayo tumika na wadau muhimu wa kuboresha biadhaa
hizi.
“Kongamano
hili la kitaalamu la wadau likiwa ni moja ya shughuli za uzinduzi wa Jukwaa la
ubunifu wa bidhaa za mimea dawa kwa maendeleo ya taifa litajikita Zaidi kwenye
kujadili Uboredhaji wa uzalishaji,uchakataji,ufungsdhsji na uuzaji wa bidhaa
zinazotokana na mimea dawa hapa Tanzania na namna ya kutatua changamoto hizo”
Alisema Dkt. Mabiki.
Kwa upande wake Mkuu wa Ndaki ya Solomoni Mahlangu ya Sayansi
na Elimu Dkt. Geofrey alisema kwa upande
wa utafiti ndaki hiyo
ni ya pekee inayotoa shahada ya uzamili ambazo zinajikita moja kwa moja katika
utafiti wa mazao ya mimea dawa ambayo mojawapo inahusika katika tukio hili na
ina miradi Zaidi ya tisa ambayo kwa namna moja au nyingine zinagusa bidhaa hizi
za mimea dawa.
“Kwa sababu
hiyo tunategemea kuchangia juhudi za SUA na Taifa katika kuongeza ubora wa
bidhaa hizi ili zipate Masoko” Alisisitiza Dkt. Kalugila.
Pia Dkt. Geofrey
Kalugila aliwashukuru wadau hao kutoka maeneo yote nchini kufiki akushiriki
kwenye kongamano hilo,maonesho na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu na kuwataka
watumia siku chache watakazokuwa SUA kujifunza na kujionea mambo mbalimbali ya
kistoria kwenye kampasi hiyo ambayo ilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa Afrika
kusini.
Kongamano hilo litafuatiwa na Maonesho makubwa ya Tiba asili na bidhaa zake litakalofanyika kwenye viwanja vya soko kuu la mkoa wa Morogoro tarehe 22/01/2021 na baada siku ya jumamosi kutakuwa na uzinduzi wa Jukwaa la ubunifu wa bidhaa za tiba asili litakalofanyika kwenye kampasi ya Solomon Mahlangu Mazumbu tarehe 23/01/2021 zilizoandaliwa na Mradi wa GRILi.
No comments:
Post a Comment