Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
Tanzania kwa kushirikiana na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), leo
imetangaza kuzindua huduma ambayo inawapa nafasi Wateja wa Airtel Money
kufungua akaunti zao za biashara, kununua na kuuza hisa, IPO na kupokea
malipo kupitia akaunti zao za Airtel Money
Applikesheni hiyo (MTP)
inayojulikana kama ‘Hisa Kiganjani’ imeanzishwa kwa lengo la kurahisisha
shughuli za uwekezaji kwa wawekezaji kupatikana moja kwa moja na
kuwekeza katika soko la Hisa la DSE.
Ubunifu huu unatarajiwa kuongeza ufanisi wa kibiashara kwa wawekezaji waliopo sasa na kuongeza wawekezaji wapya ambao kwa sasa hawahudumiwi kwa sababu ya kutopatikana kwa jukwaa la biashara ya dhamana ya DSE.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda amesema kuwa “jukwaa la DSE Mobile Trading ni alama mpya ya kuboresha uzoefu kwa wawekezaji.
"Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE) kwa kushirikiana na
wadau wa maendeleo ya huduma za kifedha (FSDT) na Serikali imeweza
kutengeneza mfumo wakiditali wa Mobile Trading Platform yaani (MTP).
Sasa ushirikiano wa DSE na Airtel Money kama mtoa huduma anayeongoza kwa
kutoa huduma za fedha kwa njia simu za mkononi, inatoa fursa kwa
Watanzania kuwekeza kupata huduma hizi kwa Airtel Money ambapo mteja
anaweza akafungua akaunti ya biashara ya Soko la Hisa la Dar es Salaam
(DSE), akanunua au kuuza hisa pamoja na kupokea malipo.
“Airtel
Money siku zote tumekuwa tukizindua huduma ambazo ni za kiubunifu zaidi
ili kutimiza mahitaji ya kila siku ya wateja wetu, kwa mfano sasa wateja
wanaweza kufanya malipo na bili tofauti kwa urahisi zaidi na sasa
Airtel Money inazindua huduma ya kununua kwa kupitia Airtel Money ambayo
ni rahisi salama itawawezesha wateja wa Airtel Money kununua hisa na
IPO kupitia Airtel Money kwa urahisi muda wowote ule bila mipaka,
alisema Nchunda huku akiongeza kuwa vijana na wazee sasa wamepata
suluhisho wakitaka kuwekeza na wakati huo huo kuokoa muda kadri
iwezekanavyo,
Nchunda alisema ili wateja wa Airtel kufurahia huduma hii, wanatakiwa wafuate njia zifuatazo,
• Piga *152*00#
• Changua malipo ya serikali
• Changua DSE
• Changua nunua hisa
• Changua herufi ya kampuni
• Changua kampuni ya kununua
• Ingiza idadi ya hisa za kununua
• Ingiza bei ya kununua
• Changua dalali wa kununua
• Ruhusu dalali atume tena oda yako
• Changua ndio
• Changua akaunti inayonunua
• Ingiza CSD PIN
• Endelea na malipo
• Changua ndio
“Airtel tunafuraha kubwa sana kuingia kwenye ushirikiano kama huo ambao unaongeza thamani kwa wateja wake. Tunafurahi kuingia katika ushirikiano na Soko la Hisa la Dar es Salaam. Hii itaongeza thamani kwa huduma zetu zilizopo kwa faida ya wateja wetu, ambapo wateja wetu wataweza kufanya biashara kwa kutumia simu zao za mkononi.
Kwa kuongezea, katika kuunga
mkono ajenda ya serikali kuleta suluhisho la kifedha kupitia kuwezesha
malipo ya kidijitali kama hii ya ununuzi wa hisa na IPOs. Natoa wito kwa
wateja wetu kutumia huduma ili kuokoa muda na kuwekeza wakiwa mahali
popote wakati wowote.” alisema Nchunda.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Baishara wa DSE Ibrahim Mshindo ilisema kuwa Hisa Kiganjani inalenga kurahishisha kazi ya uwekezaji pamoja na wawekezaji kupitia kukuza upatikanaji wa moja kwa moja wa jukwaa la soko la hisa la DSE.
Ubunifu huu wa Hisa Kiganjani ni imani yetu kuwa utaongeza ufanisi
zaidi kwenye biashara kwa wawekezaji waliopo na kuleta wawekezaji
wapya, ambao kwa sasa hawakupata nafasi ya kununua hisa zaidi au
kuhudumiwi kwa sababu ya kutopatikana kwa jukwaa kama hili la DSE.
Aliongeza kuwa la "DSE Hisa Kiganjani App na USSD" lina huduma za usalama ambazo zinaruhusu wateja kufanya shughuli salama.
'Hisa Kiganjani ina faida
kadhaa ambazo ni pamoja na, upatikanaji rahisi wa bidhaa na huduma,
kupunguza gharama za usafiri na upatikanaji wake kwa urahisi, itaongeza
uwazi na usalama wa wawekezaji.
Alisema kuwa ili mtu apate sifa ya kununua hisa ni lazima awe Mtanzania, anapaswa kuwa na Kitambulisho cha Taifa cha NIDA, anapaswa kujiandikisha kwa DSE kupitia simu kwa ussd au Applikesheni ya DSE na mwisho awe na Airtel Money akaunti yenye fedha.
No comments:
Post a Comment